umefanyika uzinduzi wa minada ya mbaazi msimu wa 2023/2024 katika wilaya ya Tunduru katika kijiji cha majimaji tarehe 12.08.2023.
Katika uzinduzi huo pia Chama kikuu cha ushirka wilaya ya Tunduru (TAMCU LTD) kimeendesha mnada wa kwanza wa zao hilo la mbaazi ambapo , kilo 839,941 ziliingia sokoni kwaajili ya kuuzwa katika mnada huo.
Aidha wanunuzi ishirini (20) waliomba zabuni ya kununua mbaazi hizo zilizopo ghalani kwa mnada wa kwanza ,na wanunuzi watatu walishinda kununua mbaazi zote zilizopo ghalani tani 839,na kufanya bei ya juu kuwa shilingi 20,18/= na bei ya chini kuwa shilingi 2,015/= na bei wastani kuwa 2,016/= ,na kufanya Zaidi ya bilioni 1.6 kuingia katika mzunguko wilaya ya Tunduru.
Katika uzinduzi huo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD ) Ndg. Mussa Manjaule aliwaomba wakulima kuendelea kulima na mazao mengine mbadala na si kutegemea zao moja la biashara kama ilivo katika maeneo yetu zao la korosho, na kuendelea kujituma na kuendelea kutanua mashamba ,kama inavofahamika kipaumbele chetu kikubwa na kilimo katika wilaya yetu ya Tunduru.
Pia afisa ushirika wilaya ya Tunduru Ndg George Bisani , amesisitiza chama kikuu na vyama vya msingi kuwalipa wakulima kwa wakati pale tu wanunuzi wanapoingiza fedha hizo. “hakuna sababu ya kuchelewesha fedha za mkulima” na amewataka watendaji wa vyama vya msingi kuendelea kuwa waaminifu na waadilifu wanapohudumia wakulima.
Kwa upande wao wakulima wameendelea kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya msimamizi wake RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mfumo huu wa uuzaji mazao kwa stakabadhi ghalani kwani ni mfumo wenye tija kwa pande zote mbili za mnunuzi na mkulima ,na na kuendelea kuiomba serikali sikivu kuusimamia mfumo huo ili uzidi kuleta tija Zaidi kwa wkaulima.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.