Wakulima wa Mbaazi wilaya ya Tunduru wameingiza zaidi ya bilioni 10 katika mauzo ya zao la Mbaazi kwa njia ya Stakabadhi ghalani, baada ya kufanyika kwa minada mitano ya zao hilo kwa msimu wa 2023/2024.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Meneja mkuu wa Chama kikuu cha ushirika Tunduru Ndg .Imani Kalembo Septemba 29, 2023, amesema kwa msimu huu wa mauzo ya zao la Mbaazi Chama Kikuu kimefanikiwa kufanya minada mitano, ambapo tani zisizopungua 5,000 zimeuzwa katika minada hiyo, na kufanya zaidi ya shilingi bilioni 10 kuingia katika mzunguko wilayani Tunduru.
“kumekuwa na ongezeko kubwa la bei kwa msimu huu wa mbaazi ukilinganisha na msimu uliopita 2022/2023” Alisema “Ambapo bei ya wastani ilikua shilingi 868 ukilinganisha na msimu huu ikiwa shilingi 1,998”
Aidha, Meneja Kalembo amepongeza na kushuru jitihada zinazo endelea kuoneshwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan Pamoja na Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe, katika kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na mfumo huu wa Stakabadhi ghalani kwa kuondoa wanunuzi wa kati wa mazao hayo machanganyiko ,pia amemshukuru kwa dhati Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Wakili, Julius S. Mtatiro kwa kujitoa kwake kuwatetea wakulima wa mazao hayo ya Ufuta,Mbaazi na Korosho.
Meneja Kalembo amesema matarajio ya Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru ni kukusanya zaidi ya tani 8,000 kwa msimu ujao wa zao la mbaazi, kutokana na mikakati iliyowekwa na kuahidi kuzalisha mazao yaliyo bora ya Stakabadhi ghalani ikiwemo Ufuta, Mbaazi na Korosho.
Msimu huu wa 2023/2024 kwa upande wa zao la Ufuta, Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru kilikusanya zaidi ya tani 4000, ikiwa ni zaidi ya ukusanyaji wa zao la Ufuta kwa msimu wa 2022/2023, ambapo kwa msimu wa 2023/2024 zao hilo limewaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 17.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.