Meneja wa bodi ya korosho tawi la wilaya ya Tunduru , ndug Shauri mwakiwa , amewasihii na kuwashauri wakulima wa korosho katika wilaya ya Tunduru katika mwendelezo wa vikao vya ushirika , kuwa , wanatakiwa kwa msimu ujao kuchangamkia soko la korosho zilizobanguliwa kuliko kushiriki sana na soko la korosho ghafi kwasababu kwa sasa limeshuka sana .
Pia amesema kuwa serikali kupitia bodi ya korosho itawasaidia wakulima katika upatikanaji wa mashine za kubangua korosho ili ziwawezeshe katika kufikia soko hilo la korosho banguliwa ,kwasababu masoko ya korosho banguliwa ni mengi sana.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.