Leo, Agosti 27, 2025, Ndg. Bosco Oja Mwingira, Msimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo ya Tunduru Kaskazini na Kusini, ametangaza majina ya wagombea walioidhinishwa kugombea viti vya ubunge katika majimbo hayo.
Amevitaja vyama hivyo ikiwa ni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wagombea wake ni Ndug. Sikudhani Yassini Chikambo-Tunduru Kaskazini na Ndug.Fadhili Sandali Chilombe, Chama Cha Wananchi (CUF) wagombea ni Ndug. Rashid Yassin Swaleh-Tunduru Kusini na Ndug.Halifa Mohamed Lulanga-Tunduru Kaskazini, Chama cha ACT-Wazalendo Wagombea Wake ni Ndug. Ado Shaibu Ado-Tunduru Kaskazini na Ndug.Mtutura Abdallah Mtutura-Tunduru Kusini, Chama Cha Wakulima (AAFP) Kina Mgombea Mmoja Ndg.Fatuma Ausi Salumu kutoka Jimbo la Tunduru Kaskazini na Chama Cha Ukombozi (CHAUMA) Wagombea wake ni Ndug. Juma Seif Said.
Uteuzi huu umefanywa baada ya uhakiki wa fomu za wagombea na kuhakikisha wametimiza masharti yote ya kisheria yanayohitajika. Taarifa hii muhimu imebandikwa kwenye ubao wa matangazo uliopo katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi ili wagombea na wananchi waweze kupata taarifa hizo kwa urahisi.
Uteuzi wa wagombea ni hatua muhimu katika mchakato wa uchaguzi. Kulingana na sheria za uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi anawajibika kupokea fomu za wagombea, kuzihakiki, na kutangaza majina ya wale waliofaa kugombea. Lengo kuu la mchakato huu ni kuhakikisha kuwa wagombea wote wanaokidhi vigezo vya kisheria ndio wanaoruhusiwa kuendelea na kampeni.
Baada ya hatua hii, wagombea walioidhinishwa wataruhusiwa kuanza kampeni rasmi za uchaguzi ili kuomba ridhaa ya wananchi wa majimbo ya Tunduru Kaskazini na Kusini. Ni muhimu kwa wananchi kufuatilia kwa karibu mchakato huu na kuwajua wagombea wao ili waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura.
Aidha, Kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025.
Kauli mbiu ikiwa “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.