Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kupitia maagizo ya Mwaka 2008 hadi 2011 kutoka Serikali Kuu ilitenga Vitalu 279 katika Kata 8 amabazo ni Tinginya, Mindu, Muhuwesi, Misechela, Jakika,Nandembo,Ligunga na Namakambale ambavyo Vitalu hivyo upatikana katika Vijiji 11 ikumbukwe wakati huo wa kuunda Vitalu hivi Jamii husika ilishirikishwa kikamilifu katika mikutano na vikao mbalimbali.
Dc Mtatiro kupitia Kikao Cha Baraza la Madiwani amewataka Wafugaji wote kurejea katika Vitalu amabavyo walipangiwa ili kuepusha migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji kwani ukizingatia kipindi hiki cha Kilimo na asili ya Wilaya ya Tunduru ni Kilimo na sio Ufagaji wa Makundi makubwa ya Mifugo.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Msomi Julius Mtatiro aliendelea kusema “Wafugaji wasiofuata Mwongozo na kanuni za Wizara ya Mifugo ikiwemo kuwataka Wafugaji walipie Vitalu ambavyo wanatakiwa waishi na Mifugo yao, kwa Mfugaji ambae hatalipia Vitalu na kutokaa kwenye kitalu huyo atatakiwa kuondolewa Tunduru na aelekee nje ya Mkoa wa Ruvuma kwani kwa Mkoa wa Ruvuma ni Halamashauri ya Wilaya ya Tunduru Pekee iliyotenga Vitalu”.
Aidha Dc Mtatiro aliwaeleza Madiwani kuwa “Operesheni ya Mifugo itakuwa endelevu mpaka pale Wafugaji watakapo tambua wajibu wao wakukaa kwenye Vitalu na Kuvilipia pia Dc Mtatiro alitoa Onyo Kali kwa Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji wanaojichulia sheria mkononi ya kuwakaribisha Wafugaji kwenye kijiji bila ya Wanakijiji kushirikishwa, pia ukizingatia Kijiji hakina eneo lililo tengwa kwajili ya Vitalu”.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.