Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeendesha mafunzo kwa Viongozi ngazi ya kijiji,kitongoji na Mtaa, mafunzo hayo yalifanywa kuanzia Oktoba 09 -10, 2023.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo juu ya Usimamizi wa fedha, uibuaji na usimamizi wa Miradi na utaratibu wa manunuzi. Mafunzo hayo yalisimamiwa na idara ya Maliasili na Hifadhi ya Mazingira.
Pichani (Aliyesimama): Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi (W) Tunduru Ndg, Dunia Almasi
Mafunzo hayo yamekuja baada ya vijiji hivyo kuanza kupokea fedha za awali zitokanazo na biashara ya Hewa Ukaa, ambapo, Vijiji vipatavyo 21 vimeingia katika biashara hiyo. Vijiji 10 kutoka jumuiya ya uhifadhi ya Narika na Vijiji 11 kutoka jumuiya ya uhifadhi Chingoli, ambapo hadi sasa vimepokea jumla ya fedha shilingi milioni 27.
Akizungumza ofisini kwake Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi (W) Tunduru Ndg, Dunia Almasi, ametoa rai kwa wanajamii na jamuiya za uhifadhi kuendelea kutunza Maeneo ya misitu, kwani imekuwa ni moja ya kichocheo cha maendeleo hasa katika vijiji.
“Jamii zetu zimetunza haya maeneo ya misitu, jamii inakwenda kunufaika na shughuli za maendeleo na kuweza kutatua kero zitokanazo na Mazingira”. Alisema.
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inatarajia kuingia mkataba ili kuanza kufanya biashara na mwekezaji wa Biashara ya hewa ukaa, ambapo vijiji vipatavyo 21 vinatarajiwa kuingia katika bishara hiyo, vijiji hivyo vinatoka katika jumuiya mbili za uhifadhi zilizopo wilayani Tunduru ambazo ni Narika na Chingoli.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.