Afisa Ushirika (w) Tunduru Ndg George N. Bisani ametoa Elimu na kufanya ukaguzi wa kawaida wa uandishi wa vitabu vya kihasibu kwa Bodi na Watendaji wa Vyama vya Msingi katika Wilaya ya Tunduru.
Lengo kuu likiwa na kusaidia kupunguza hoja za ukaguzi na kuangalia mwenendo wa shughuli za Ushirika katika vyama hivyo,ambapo Bisani amevitaka vyama vya Msingi vya Ushirika kuzingatia majukumu yao na kuyatimiza kwa kufuata sharia na taratibu zilizowekwa na Tume ya ushirika Tanzania
Bisani amesema , mpaka sasa vyama 14 vimeshafikiwa katika ukaguzi huo kati ya vyama 37 vya msingi vya Ushirika vilivyopo katika Wilaya ya Tunduru, na amesisitiza uhuishaji wa taarifa za vyama katika Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU), na kuwataka kutunza nyaraka zote muhimu za vyama vya Ushirika vya Msingi.
Pichani, ni Afisa Ushirika (W) Tunduru Ndg George Bisani akizungumza wakati akitoa Elimu na kufanya ukaguzi katika Vyama vya Msingi.
“Ushirika unaendeshwa kwa utaratibu na kanuni na unahitaji msingi wa ushirikishwaji”,Alisema . “Ninyi kama wasimamizi wa Ushirika, yapaswa kutimiza majukumu yenu kikamilifu na kwa uaminifu Mkubwa”.
Bodi na watendaji wa vyanma vya msingi wamemshukuru Afisa ushirika kwa kuwapa elimu yenye tija ambayo inakwenda kuwanufaisha katika usimamizi wa vyama vya msingi , na kuahidi utekelezaji wa yale yaliyoelezwa na Afisa ushirika.
Pichani ,ni Baadhi ya wajumbe wa Bodi na watendaji wa vyama vya Msingi vya Ushirika wakiwa katika mafunzo na Afisa Ushirika wilaya ya Tunduru.
Tunduru ni moja ya wilaya ambayo wakulima wa mazao ya Korosho, Ufuta na Mbaazi wanauza mazao yao kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani, ambapo kwa sasa inajiandaa na Minada ya uuzaji wa zao la Korosho,inayotarajiwa kuanza mnamo Oktoba 26,2023.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.