wananchi wa Kijiji cha Muungano kilichopo Wilayani Tunduru katika Kata ya Mtina wakitoa hoja wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mapema wiki katika viwanja vya ofisi ya kijiji hicho, wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo kuu la kusikiliza kero,maoni na ushauri wa wananchi kwa serikali katika kutekeleza dhana ya uwajibikaji na utawala bora.
Aidha waliulalamikia uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa kutokutekeleza majukumu yao ipasavyo na migogoro iliyomo kati viongozi hivyo kuchelesha shughuli za maendeleo katika kijiji chao hivyo kuuomba uongozi wa wilaya kuwasaidia kuwajengea uwezo viongoi wa kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi mwakilishi kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Kaimu Afisa Utumishi wilaya ndg Juma Ally alisema ni vyema wananchi kutambua kuwa nafasi za viongozi waliowachagua na kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao na kauli mbiu ya serikali inamtaka kila mwananchi kufanya kazi na ili kujenga uchumi wa viwanda ni jukumu la kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na shughuli za maendeleo na kufanya kazi zitakazowaongezea kipato.
Ndg Juma aliendelea kusema kuwa ni kuna utaratibu wa kuchagua na kumuondoa kiongozi yeyote madarakani kwa kuzingatia sheria ya kuanzishwa kwa mamlaka za serikali za mitaa hivyo ni vyema wananchi wakafuata taratibu hizo na sio kujichukulia uamuzi tu wa kumtoa na kutengua uongozi uliopo madarakani bila ya kuzingatia sheria na 2 ya mwaka 1982 ya kuanzishwa mamlaka za serikali za mitaa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.