Serikali kupitia Bodi ya korosho Tanzania itagawa bure viuatilifu kwa wakulima wa korosho,ugawaji huo wa viuatilifu kwa msimu huu utafanyika kwa njia ya kupitia kwa vyama vikuu vya ushirka na vyama vyake vya msingi kwenda kwa wakulima wa korosho,kuptia mfumo wa kidigitali wa upokeaji na ugawaji viuatilifu .
Kwa kutambua umuhimu wa jambo hili Bodi ya korosho wilaya ya Tunduru kupitia kwa meneja wake Bi shauri Mokiwa waliandaa mafunzo maalumu kwa meneja wote wa vyama vya msingi ili kujifunza matumizi sahihi ya mfumo huo wa upokeaji na ugawaji wa viuatilifu katika wilaya ya Tunduru.
Katika mafunzo hayo yalihudhuriwa na katibu Tawala wilaya ya Tunduru Ndg. Augustino Maneno ,aliwaomba mameneja wa vyama vya msingi kuzidikuwasaidia wakulima katika kuwapa elimu hasa ya huu mfumo wa upokeaji na ugawaji viuatilifu na pia elimu juu ya utumiaji sahihi na uhakika wa viuatilifu ili kuweza kuwa na uzalishaji wenye maslahi ya mkulima na ukuzaji wa uchumi.
Aidha alivitaka vyama vya msingi ambavyo vimeanza kupokea zao la ufuta ,kulinda ubora wa ufuta huo kwa kutoruhusu uingizwaji wa ufuta ulio na uchafu katika maghala yao ili kuvutia wanunuzi kuweka bei nzuri katika minada inayokuja hivi karibuni.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.