Bilioni 1.5 zimejenga shule tatu mpya za sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika kata tatu ambazo ni Kata ya Nakayaya, Kata ya Majimaji na Kata ya lukumbule.
Ujenzi wa shule hizo ulikamilika na kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wapatao 500 kwa mwaka huu wa masomo 2023 – 2024.ambazo ni shule ya Sekondari Kungu, shule ya sekondari Majimaji na Shule ya Sekondari Mpakate
Fedha hizo zililetwa kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika wilaya ya Tunduru ,aidha wananfunzi wanufaika wa miundombinu hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.