Benki ya Tanzania (BOT) tawi la Mtwara imefanya semina ya uwekezaji wa dhamana katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru. Semina hii ililenga kuwajengea uelewa wananchi kuhusu fursa za uwekezaji kwenye dhamana za serikali, utaratibu wa minada ya dhamana za serikali pamoja na faida zake.
Semina hiyo iliwezeshwa na wataalamu kutoka Benki ya Tanzania, ambao walitoa maelezo ya kina kuhusu: aina mbalimbali za dhamana zinazopatikana, Walieleza faida lukuki za kuwekeza kwenye dhamana, Walitoa maelekezo ya wazi kuhusu jinsi ya kuwekeza kwenye dhamana, vile vile, Walisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Aidha, Akizungumza wakati wa semina hiyo Ndg. David Mponeja, Meneja wa Fedha na Utawala kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Mtwara alieleza kuwa wananchi wanapaswa kufahamu jinsi ya kutunza fedha ma namna sahihi ya kuzitumia taasisi za Fedha ili kuweza kutekeleza sera ya Fedha.
Semina ya uwekezaji wa dhamana kutoka Benki ya Tanzania katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ilikuwa ni hatua muhimu katika kuwajengea uelewa wananchi kiuchumi. Inatarajiwa kuwa, semina hiyo itakuwa chachu ya kuongeza uwekezaji na kuchochea maendeleo katika wilaya.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.