Mkuu wa wilaya ya Tunduru mh.Juma Zuberi Homera afanya ufunguzi darasa la kisomo katika za msingi Mbesa na Airport zilizopo kata ya Mbesa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Akitoa hotuba kwa wanakisomo hao mh Homera alisema kuwa elimu ya watu wazima itasaidia wanakisomo kupata haki zao za msingi ikiwa watakujua kusoma,kuandika na kuhesabu hivyo kuondokana na adui ujinga katika taifa la Tanzania .
Pia kwa wananchi kupata elimu hii amabyo waliikosa kwa muda mrefu itasaidia hata katika uchaguzi wa mwaka 2020 kushiriki na kumpigia kura kiongozi unayemtaka bila ya kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kujua kusoma na kuandika.
kutokana na senza iliyoafanywa na TASAF imegundulika kuwa wilaya ya Tunduru ina jumla ya watu wasiojua kusoma na kuandika ni asilimia 30, hivyo kupunguza kasi ya ushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kushindwa pia kujua namna ya kupata haki zao kutokana na ukosefu wa elimu.
vilevile kutokana na mila na desturi za jamii ya Tunduru takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya wasiojua kusoma na kuandika ni wanawake hivyo jamii inatakiwa kuondoa dhana potovu iliyojengeka miongoni mwao kuwa watoto wa kiume ndio wenye fursa ya kupata Elimu na wale wa kike wakiwaacha kwa ajili ya kuolewa na kufanya kazi nyingine za nyumbani.
akitoa taarifa hiyo mbele ya mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Zuberi Homera afisa Elimu Takwimu na vielelezo ndg Abdul Kazembe alisema kuwa jamii ya Tunduru inakabiliwa sana na mfumo dume na wanawatenga sana watoto wakike hivyo kumuomba mkuu wa wilaya kuhamasisha wananchi kuona umuhimu wa watoto wa kike kupata Elimu kwani wana Haki sawa na watoto wa kiume.
aidha akisoma risala kwa mgeni mkuu wa shule ya msingi mbesa alisema kuwa changamoto kubwa wananyokumbana katika kuendeleza darasa la kisomo ni miundombinu ya kufundishia ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme katika shule za msingi Aiport na Mbesa, ukosefu wa darasa la wanakisomo, ukosefu wa deki na Tv kwa ajili ya kufundishia kwani ufundishaji wa watu wazima nio tofauti na elimu ya awali.
Akitoa ufafanuzi wa changamoto hizo mkuu wa wilaya Mh.Juma Zuberi Homera aliipongeza halmashauri ya wilaya ya tunduru kwa kuona umuhimu wa kuanzisha darasa la wanakisomo ili kupigana vita na adui ujinga na kuwasaidia wananchi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, hali hii itachochea maendeleo katika wilaya yetu na kuendana na kauli sera ya serikali ya kuboresha elimu na kutoa elimu sawa kwa wote.
Mh. homera aliguswa sana na muamko wa wananchi walijitokeza kusoma hivyo kuahidi kutoa mchango wa bati 30 kwa ajili ya kuuzeka darasa la wanakisomo, kuwapelekea wanakisomo Deki na TV ili waweze kujifunza katika mazingira wezeshi na rafiki.
Aidha kwa upande wa changamoto ya Umeme mkuu wa wilaya aliugiza uongozi wa shule kushirikiana na viongozi wa kata ili kuhakikisha kuwa umeme unafungwa katika shule ya msingi Mbesa na Airport kwa haraka.
Hata hivyo wanakisomo waliishukuru srikali kwa kuanzisha darasa la wanakisomo katika kata yao ya mbesa kwani inawasaidia kuongeza maarifa na kujua namna ya kuweza kupata huduma zao kwani wengi wao walikua hawajui kusoma na kuandika kabisa, na kuwaomba uongozi wa halmashauri kuanzisha na sehemu nyingine ili wananchi wengi wanufaike na huduma kama wanayoipata.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.