Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii leo tetehe 07/08/2017 imefanya mkutano wa kuanza mchakato wa kuanzisha jukwaa la uwekezaji wanawake kiuchumi katika ukumbi wa Boma.
Kufuatia agizo la makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hasan la kila halmashauri kuanzisha jukwaa la uwekezaji wanawake kiuchumi.
Aidha jukwaa hili litaunganisha wanawake kutoka kada tofauti tofauti na kutoa fursa za Uchumi, Biashara,upatikanaji wa mitaji, na kupitia sheria za nchi katika masuala ya Uchumi na jinsia ya kujitegemea kiuchumi.
Aidha akifanya mkutano wa kwanza na wanawake wa wilaya ya Tunduru wanaounda jukwaa la wanawake mratibu wa uwezeshaji dawati la kiuchumi wilaya Ndg Fadhili Muhamed Chidiyaonga alisema jukwaa la wanawake wilaya litawawezesha wanawake wa wilaya ya Tunduru kuongeza fursa za kiuchumi na kuwa na maisha yaliyo bora na kuwa kama wanawake wa maeneo mengine nchini.
Vilele alisema ili kuweza kuendesha jukwaa hill la wanawake in lazima wapatikane viongozi na wajumbe watakaosimamia jukwaa hilo, ambapo walifanya uchaguzi wa mwenyekiti, Katibu na mhasibu pamoja na wajumbe saba 7 watakaofanya kazi kwa kushirikiana na Halmashauri.
Viongozi waliochaguliwa ni pamoja na mwenyekiti ambaye ni bi Fatima Rajabu Mkina, katibu bi Asigele Chonde, mhasibu bi Sarah Joseph Pili pamoja na wajumbe saba.
Baada ya uchaguzi huo kukamilika mratibu wa dawati la Uchumi wilaya ndg chidhaonga alisema kuwa viongozi HAWA wanaanza Nazi Mara moja ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi wa Tunduru .
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.