Uyoga ambao tunaufurahia kwenye mlo wetu sio lazima utoke porini tu. Teknolojia ya kisasa imetuwezesha kuzalisha uyoga kwa wingi na ubora wa hali ya juu katika mazingira yaliyodhibitiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imekuletea Uyoga huu ambao uaweza tumika kama chakula.
Uyoga huu umefuata Mchakato ufuatao wa Uzalishaji:
1. Kianzio kutoka Maabara: Safari ya uyoga huanza katika maabara. Kimelea kidogo cha uyoga, ambacho kimekuwa kikilindwa kwenye chupa, hutumika kama kianzio cha uzalishaji. Kimelea hiki kina uwezo wa kuzaa mamilioni ya uyoga.
2. Maandalizi ya Shamba: Baada ya hapo, kimelea hiki kinapelekwa kwenye shamba maalumu la kuoteshea uyoga. Shambani, mabaki ya migomba yaliyokauka huandaliwa kwa makini. Mabaki haya huozeshwa kwa kumwagiliwa maji ili kuunda mazingira yenye unyevunyevu ambayo uyoga hupenda.
3. Kuota kwa Uyoga: Kimelea kutoka maabara huwekwa kwenye mabaki ya migomba yaliyokauka na kuandaliwa. Kwa siku 7 hadi 14, kimelea hiki huanza kuota na kuenea
4. Mavuno: Baada ya takriban siku 21, uyoga huwa tayari kuvunwa na kuliwa. Uyoga huu uliotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa huwa na ubora wa hali ya juu na unakuwa tayari kutumika katika mapishi mbalimbali.
Je, ungependa kujionea na kujua zaidi kuhusu uyoga huu toka Tunduru? Karibia Banda letu ukutane na wataalamu wetu ambao wapo tayari kujibu maswali yako yote.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.