Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kalulu wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, katika ziara ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera alisema serikali katika awamu tofauti imetekeleza mbali mbali ya maendeleo katika kata na vijiji vya halmashauri ya Tunduru.
Mh. Homera katika taarifa yake alisema kuwa katika sekta ya maji kata ya kalulu vijiji vya mbungulaji na rahale vimechimbwa visima vya ambapo kisima cha mbungulaji kilichowekwa jiwe la msingi na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania Kasimu Majaliwa wananchi wanapata maji lakini kisima cha kata ya kalulu serikali imeongeza fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa kazi katika eneo ambalo maji yatapatikana kwa wingi.
Pia aliendelea katika sekta ya elimu uboreshaji wa miundombinu ya Elimu inaendelea kuboreshwa na Kata ya Kalulu shule ya msingi kalulu iliyopo kijiji cha rahaleo serikali inaendelea na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, ofisi moja na matundu nane ya vyoo ambapo mradi huu umegharimu jumla ya shilingi milioni 66,600,000 zilizotolewa na mfuko wa elimu wa matokeo makubwa EP4R, lakini katika kukabiliana na uhaba wa watumishi katika sekta ya elimu halmashauri imepokea jumla ya walimu 66 ambao wanaendelea kuripoti na shule ya msingi Kalulu ni mojawapo ya shule walizopangiwa walimu.
Naibu waziri wa Maliasili Utalii Mh. Japhet Hasunga akiongea na askari wanyamapori Kanda ya Kalulu wakati wa ziara ya ufuatiliaji na uendelezaji wa Vivutio vya Utalii na Malikale mikoa ya kanda ya Kusini.
Juma Homera aliendelea kusema kuwa katika kuboresha ubora wa huduma za afya serikali imeendelea kuajiri watumishi wa afya, halmashauri ya tunduru impangiwa jumla ya watumishi wa afya 90 ambao watapangiwa katika zanahati na vituo vya afya na zahanati ya Rahaleo ni watapangiwa mtumishi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, lakini pia serikali inaendelea na upanuzi wa majengo katika kituo cha afya kilichopo makao makuu ya tarafa Matemanga ili huduma za mama na mtoto, upasuaji mdogo, na upatikanji wa mashine ya mionzi ya kupima ujauzito (Ultrasound).
Aliendelea kusema kuwa serikali inaendelea na usambazaji wa umeme vijijini REA III na kijiji cha rahaleo na mbungulaji vipo katika mpango huu, hivyo niwatake wananchi kutumia fursa ya kufika kwa umeme katika kata ya Kalulu kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuweza kujiendeleza kiuchumi na kukuza kipato.
vilevile Mh. Homera aliwataka wananchi wa kata kata ya Kalulu kujikita katika kilimo cha zao la ufuta ili kuweza kushiriki kwa ukamilifu katika msimu ujao wa mazao mchanganyiko na kuingia katika mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo mikoa ya Lindi na Mtwara kwa Mwaka huu walifanikiwa sana.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Tunduru aliwataka wananchi wa kata ya Kalulu kutokulima mazao yanayopendwa na wanyamapori kama Ndovu na Tembo ili kuepuka mazao yao kuliwa na wanayama hao, pia wananchi kutokufanya kilimo kando kando na hifadhi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.