Hayo yamesemwa na wananchi wa kijiji cha Mpanji wakati wa kikao cha kujadili njia za kupambana na wanyama hao ambao wamevamia miradi ya mabwawa ya samaki iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18 na mwaka 2018/2019.
Miradi hii ya ufugaji wa samaki katika mabwawa ni miongoni mwa miradi mingi inayotekelezwa na Mpangi ikiwa na lengo la kuongeza kipato kwa wanufaika wa kaya maskini wilayani Tunduru ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Akitoa taarifa ya uharibifu uliofanywa na wanyapori katika mabwawa ya kufugia samaki Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mpanji Bwana Joseph Juma alisema tembo wameanza kuingia katika maeneo ya mabwawa ya kufuga samaki toka tarehe 19/04/2019 mpaka sasa ambapo hufika kila baada ya siku mbili.
katika picha ni muonekano wa bwawa la kufugia samaki katika kijiji cha mpanji lililoharibiwa na tembo wanaofika katika eneo la mradi huo kwa jili ya kupata maji.
Lakini tembo hao hufika kwa makundi kuja kunywa maji katika mabwawa hayo, hali hii kwa hapo nyuma haikuwahi kutokea mpaka Februari mwaka 2019 ndio wameanza kuonekana katika maeneo mbalimbali ya kijiji ikiwemo kufika katika mabwawa hayo ya kufugia samaki.
Aidha aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha mwezi julai 2019 tembo wamekuwa wakionekana katika eneo la mradi wa mabwawa ya kufuga samaki kila baada ya siku mbili ambapo hufika kunywa maji wakiwa katika makundi hali iliyopelekea kupasua mabwawa ya kufugia samaki na hakuna tumaini la uwepo wa samaki tena.
Joseph Juma alisema wanyama hawa wamekuwa ni hatarishi kwa maisha ya wananchi wa kijiji cha Mpanji kwani hata wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo kutokana na tembo kuonekana katika eneo hilo mara kwa mara.
“mradi huu wa ufagaji wa samaki sio rafiki katika mazingira yetu kwani hauna tija na unatishia Amani na hatarishi kwa maisha ya jamii, tunashindwa hata kwenda kufanya kazi mashamabni kutokana na hofu ya kukutana na tembo kwani wanazagaa katika mazingira yetu”alisema mjumbe wa Halmashauri ya kijiji ndg Rashidi.
Timu ya wataalamu wa Tasaf kutoka makao makuu na wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wilaya wakiwa katika ukaguzi na kufa nya tathimini ya uharibifu uliofanywa na Tembo katika mradi wa ufugaji wa samaki katika kijiji cha Mpanji.
Athari kubwa iliyojitokeza katika mradi wa ufugaji wa samaki katika mabwawa ni kupoteza samaki waliokuwa waanze kuvunwa, kupoteza Imani na mradi wa bwawa la samaki.
Kwa upande wake kaimu Afisa wanyapori wilaya Bw. Dunia Almasi alisema sababu kubwa ya tembo kufika katika kijiji na kufanya uharibifu ni kutokana na kijiji hicho kupakana na hifadhi ya misitu ya Sasawala lakini pia eneo hilo lipo ndani ya ushoroba wa Seleou - Niasa hivyo ni njia ya wanyamapori.
Halikadhalika hali ya hewa ya ukame katika hifadhi inachangia Tembo kutoka katika hifadhi kutafuta maji na Tembo ana uwezo mkubwa sana wa kunusa harufu ya maji, hivyo hufika katika eneo la mabwawa kufuata maji.
Ndg Dunia aliwashauri wananchi wa kijiji cha Mpanji kutumia njia za asili ili kuwafukuza tembo mbali katoka mazingira yao ikiwa ni pamoja na kuchanganya pilipili, jivu na oil chafu katika vitambaa na kutundika katika miti kuzunguka eneo la mradi.
Vile vile kupanda pilipili kuzunguka eneo la mradi wa mabwawa ya samaki na kuweka mizingia ya nyuki ambao watakuwa walinzi wa kufukuza tembo kufika katika eneo hilo kwani pilipili ikimuingia tembo machoni huwashwa na kubadilisha njia.
picha ya pamoja ya viongozi wa halmashauri ya kijiji cha Mpanji na wataalam kutoka Tasaf makao makuu, ofisi ya mkurugenzi mtendaji baada ya majadiliano na kufanya tathmini ya uhabifu uliofanywa na Tembo katika mabwawa ya kufugia samaki.
Hata hivyo ni wakati wa serikali kuchukua hatua za makusudi kunusuru maisha ya wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi kwani imekuwa ni changamoto kubwa na hofu kwa wananchi na mali zao kwani wanyamapori hao wanaonekana katika makazi ya wananchi mara kwa mara, vilevile taasisi zinazojishughulisha na uhifadhi wa wanayamapori kutoa aelimu kwa wananchi ya njia bora za kukabiliana na wanyama waharibifu kama hawa ili miradi inayotekelezwa iwe indelevu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.