TASAF III ni muendelezo wa awamu mbili za mrdi wa kunusuru kaya maskini Nchini, mpango huu unalenga katika kumuwezesha mwananchi mwenye hali duni ya maisha kuweza kujikwamua, kupata ahueni katika masuala ya lishe, afya na elimu.
Halmashauri ya wilaya ya tunduru ni miongoni mwa halmashauri nyingi nchini mambazo zinatekeleza mradi wa kunusuru kaya maskani na katika awamu ya tatu ambayo imeanza mwaka 2014 jumla ya kaya 15,813 zilibainishwa na kuanza kunufaika na ruzuku ya afya,elimu na lishe.
Taarifa inaendelea kutanabaisha kuwa walengwa wanashiriki katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo walengwa ili kuweza kuondokana kabisa na umasikini, ikiwa ukarabari wa miundombinu, ujenzi wa vituo vya kutoa huduma za afya, na kazi nyingine kama ufugaji, kilimo na biashara ndogondogo.
Katika ajira za muda mfupi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imefanya kazi kazi mbali mbali ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti ya matunda,mbao na ile ya kutunza vyanzo vya maji kuzunguka vyanzo vya maji.
Kisima cha maji katika kijiji cha lijombo kikiwa katika hatua za ukarabati, kazi iliyofanywa kwa ushirikiano wa Idara ya maji na Idara ya maendeleo ya Jamii inayosimamia utekelezaji wa mradi kunusuru kaya maskini.
sambamba na hayo walengwa walishiriki katika ukarabati wa visima vya maji ili kurahisha upatikanaji wa maji na kawawezesha walengwa kuweza kushiriki katika shughuli za kiuchumi. "katika kile kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 tumefanikiwa kukarabati isima cha maji katika kijiji cha lijombo, utengenezaji wa lambo la kuhifadhia maji ya mvua ili kipindi cha kiangazi kurahisisha wananchi kupata maji, kusimamia uchimbwaji wa mabwawa ya kufugia samaki" alisema mrtibu wa Tasaf wilaya Ndg Muhidin Shaibu.
wanufaika wa kaya maskini wilayani Tunduru wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kazi za ajira za muda zinazotolewa na Tasaf ili kuwaongezea walengwa kipato.
Utokomezaji wa hali duni kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru unawezekana kwa viongozi kushirikiana na wananchi kwa karibu na kutoa elimu ya namna bora ya kilimo bora cha kisasa, ufugaji wa kisasa na wenye tija, hivyo wataalamu wa kilimo, mifugo na ustawi wa jamii wahamasishe wananchi kuona umuhimu wa kushiriki katika uzalishaji mali zaidi ya kuwa na mawazo kuwa serikali inafanya kila jambo
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.