Wakulima wa korosho Wilayani Tunduru wamekubali kuuza korosho zao Tani 4,017 katika mnada wa pili wa zao hilo.
Mnada huo ulifanyika katika kijiji cha Amani chama cha ushirika cha msingi CHAMANA (CHAMANA AMCOS), kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani, Novemba 09, 2023, chini ya Chama kikuu cha Ushirika Tunduru TAMCU LTD.
Wananunuzi 18 walionesha nia ya kununua Korosho Tani 4,017 ambazo ziliingia sokoni katika mnada huu wa pili, wanunuzi watano walishinda kununua Korosho hizo zilizopo ghalani kwa bei ya shilingi 1,831 kwa kilo.
Akizungumza baada ya kutangaza bei hiyo ya zao la korosho Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika TAMCU LTD Ndg. Mussa Manjaule amewasihi wakulima kutotegemea zao moja la kibiashara na kuwataka kulima kilimo cha mazao mchanganyiko, na kuviomba vyama vya msingi kulipa fedha za wakulima kwa wakati.
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika cha Mazao Tunduru Ndg . Mussa Manajaule, akizungumza katika mnada wa pili wa zao la Korosho.
“ Viongozi na watendaji wa vyama vya msingi tujitahidi kulipa wakulima ndani ya siku saba ambazo zimepangwa , kwani fedha hizo ni muhimili muhimu kwa wakulima hawa, zinakwenda kumsaidia mkulima katika mahitaji yake ya kila siku”
Kwa upande wake Mlajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma Bi. Peja Muhoja amewasisitizia viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika vya msingi kufanya majukumu yake kwa kufuata Miongozo ,sheria na kanuni zilizoweka kwa uaminifu na uadilifu,
Naye Meneja Mkuu wa Bodi ya Korosho Wilaya ya Tunduru Bi. Shauri Mokiwa amewasisistiza wakulima kuzingatia ubora na Usafi wa korosho wanazaopeleke ghalani, kwani ubora na usafi wa korosho unakwenda kuongeza thamani ya Korosho zetu katika sokoni.
Zaidi ya Bilioni 11 ziliingia katika mzunguko katika Wilaya ya Tunduru kupitia mnada wa kwanza wa zao la Korosho kwa msimu huu wa 2023 - 2024, ambapo wanunuzi 35 walionesha nia ya kununua korosho hizo tani 3,500 ambazo zilinunuliwa kwa shiliingi 1,994 kwa kilo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.