Chama Kikuu cha Ushirika wa Masoko ya Mazao Tunduru (TAMCU LTD) kimefanya Mkutano Mkuu wa 21,Mei 18, 2024, katika Wilaya ya Tunduru.
Mkutano huo ulifanyika mjini Tunduru na ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa vyama vya ushirika, na wanachama wa TAMCU kutoka vyama vya Ushirika vya Msingi vyote vilivyopo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Simon K. Chacha, alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo. Katika hotuba yake, Mhe. Chacha aliwataka viongozi wapya wa TAMCU kusimamia kwa ufanisi mambo na mikakati waliyoahidi kwa wanachama wao.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi na wanachama, na akawataka wanachama kuchagua viongozi waadilifu watakaowezesha ushirika kufikia maendeleo endelevu.
āMaendeleo ya Ushirika yanahitaji ushirikiano,uadilifu na uaminifu, hivi vyote vinatakiwa kuanza kutengenezwa na sisi viongozi wenyewe.Alisema Mhe,Chacha.
Mkutano huo ulienda sambamba na Uchaguzi wa kupata bodi mpya ya uomgozi wa chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD).
Ambapo katika uchaguzi uliofanyika, Ndg. Mussa Athumani Manjaule alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAMCU, Bodi ambayo inaundwa na wajumbe sita.
Katika hotuba yake baada ya kuchaguliwa, Ndg. Manjaule aliwashukuru wanachama kwa kumwamini tena kuwa kiongozi wao. Aliahidi kutekeleza mikakati yote ya TAMCU kwa lengo la kuimarisha ushirika na kuleta maendeleo kwa wanachama wake. Pia aliahidi kushirikiana kwa karibu na watumishi wa TAMCU ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya chama hicho.
Mkutano huo pia uliishuhudia uzinduzi wa magari mawili mapya ya mizigo aina ya Scania yaliyonunuliwa na vyama vya ushirika vya msingi vya SAMA AMCOS na NGUVUMALI AMCOS kwa ushirikiano na benki ya CRDB. Magari hayo yananatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima kutoka vijijini hadi masoko, na hivyo kuboresha maisha yao.
Kwa ujumla, Mkutano Mkuu wa 21 wa TAMCU ulikuwa wa mafanikio makubwa. Uchaguzi wa bodi mpya unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika ushirika huo, na uzinduzi wa magari mapya ya mizigo utasaidia kuboresha maisha ya wakulima katika Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
HakimilikiĀ©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.