Chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD) kimefanya mkutano maalum wa kujadili unadishwaji wa Ghala la kuhifadhia mazao, Mkutano ulifanyika Septemba 12, 2023 katika ukumbi wa Skyway Wilayani Tunduru.
Mkutano huo maalumu uliitishwa baada ya bodi ya TAMCU LTD kupokea barua kutoka kwa mmiliki wa Ghala hilo Ndg Fuad Said Abdallah ikitoa Taarifa ya kuuza ghala hilo,lililopo Bias mkabala na kituo cha kuuzia mafuta cha Mambo mazuri .
Pichani ni Mwenyekiti wa Mkutano huo,Ndg. Abubakari Khalifa (Aliyesimama).
Mwenyekiti wa TAMCU LTD Ndg. Mussa Manjaule alisema, Ghala hilo lina uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 kwa wakati mmoja ,aidha pamoja na ghala hilo kuna mzani wenye uwezo wa kupima Gari zima, Majengo ya ofisi, choo na yamezungushiwa uzio, ambapo baada ya majadiliano baina ya Chama kikuu na muuzaji ,muuzaji amekubali kuuza Ghala hilo kwa shilingi milioni 492.
“Upatikanaji wa ghala hili, unaenda kuchochea maendeleo ya chama kikuu, ni ghala ambalo litatusaidia sana katika ukusanyaji wa mazao ikiwemo Mbaazi,Korosho na Ufuta , na pia tuna matarajio ya kuongeza ghala lenye uwezo wa kukusanya tani elfu 10 kwa wakati mmoja”. Alisema
Pichani ni Mwenyekiti wa TAMCU LTD Ndg. Mussa Manjaule (Aliyesimama).
Aidha Wajumbe wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano huo Ndg Abubakari Khalifa Kazembe waliridhia ununuzi wa ghala hilo bila kupinga , kwani waliona ni jambo jema kwa sababu ya uhitaji wake katika chama kikuu kutokana na upungufu wa maghala ya kuhifadhia mazao ya wakulima.
Pichani ni baadhi ya wajumbe wa Mkutano maalumu wa kujadili unadishwaji wa Ghala.
Chama kikuu cha ushirika Tunduru kinawasihi wakulima kuendelea kukusanya na kuuza mazao yao kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani,ambao kwa sasa umekuwa mkombozi kwa Mkulima.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.