TAASISI YA KER YATOA MOTISHA KWA WANAFUNZI TUNDURU.
Taasisi ya Kalamu Education Foundation inayoshughulikia ubora wa Elimu wilayani Tunduru imetoa motisha kwa wananfunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na shule mbali mbali za serikali nchini Tanzania.
Akizungumza na wanafunzi hao Mkurugenzi Mtendaji W Ndg Abdallah H Mussa aliipongeza na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuweza kuwaunganisha wananfunzi hao pamoja na kujua namna ya kuweza kuwasaidia wale ambao hawatakuwa na uwezo wa kifedha na huduma zingine ili serikali iweze kuwasaidia.
Aidha aliwasisitiza wanafunzi hao kujitambua na kwenda kuitangaza Tunduru kwa mema na sio mabaya hivyo suala la nidhamu, bidii na kujituma katika masomo na serikali itakuwa inawafuatilia maendeleo katika shule mlizopangiwa.
"najua miongoni mwenu kuna madaktari, walimu, mawaziri, wabunge, wakurugenzi na viongozi katika nafasi mbalimbali na taifa linawategea sana na nisisitize tena nidhamu,kujituma,na bidii iwe ngao yenu"alisema Mkurugenzi Mtendaji wilaya.
Naye mwenyekiti wa taaisis ya Kalamu, Education Foundation ambaye pia ni manager masoko Airtel Tunduru Ndg Mohamed Kamilagwa alisema kuwa taasisi lengo lake ni kuongeza ufaulu na kufuta daraja sifuri katika matokeo ya kidato cha nne na kuinua kiwango cha elimu wilayani Tunduru.
Aliendelea kusema kuwa taasisi imefanya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwawezesha baadhi ya wafaulu kufanya ziara katika bunge la zanzibar, taasisis mbalimbali za elimu nchini na wakurugenzi wa taasisi ili kujifunza mbinu walizotumia kufanikiwa katika elimu na kushika nyadhifa walizonazo.
kamilagwa aliendelea kuwaasa wanafunzi kuzingatia wosia waliopewa na mkurugenzi wa kutumia jitihada za makusudi katika masomo ili kuweza kufikia malengo kwani hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kuwa na maneno mengi au kwa kulala sana alafu akategemea kufanikiwa itakuwa ndoto.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.