Hayo yamesemwa na makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine Prof Raphael Chibunda wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma katika hafla Fupi ya makabidhiano ya majengo ya kambi ya daraja mbili kwa ajili ya kuanzisha tawi la chuo hicho wilayani Tunduru, aliahidi kutoa mchango wa mifuko ya saruji 100 ili kuanzisha ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha darajambili.
Prof Chibunda alisema chuo kipo tayari kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuanza ujenzi wa zahanati katika kijiji cha darajambili ili kutoa huduma za haraka za afya kwa wananchi na wanafunzi watakaoajiunga na chuo katika kampasi ya Tunduru kwani watakuwa wananishi katika mazingira ya kijiji hicho.
“Chuo kipo tayari kutoa mifuko 100 ya saruji mkiwa tayari toeni taarifa kwa mtumishi anayebaki hapa ili taratibu za manunuzi zifanyike, zahanati itasaidia wananchi waliopo katika kijiji lakini pia wanafunzi watakaokuwa katika tawi hili na wengine ni watu wazima wenye familia zao hivyo zahanati ni lazima kujengwa”
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Mbwana Mkwanda Sudi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wakisaini nyaraka za makabidhiano ya majengo ya darajambili kwa ajili ya kunzaisha chuo cha kilimo sokoine kampasi ya Tunduru.
Aliendelea kusema kuwa sifa za kuijunga na chuo kikuu cha kilimo SUA ngazi ya cheti mwanafunzi anatakiwa kuwa na ufaulu wa kuanzia alama D nne na kuendelea katika mtihani wa kidato cha nne. “nawahamasisha wanafunzi kuanzia kidato cha I hadi IV kupigana kupata D4 ili kupata nafasi ya kusoma katika chuo cha SUA tawi la Tunduru”alisema Prof.Chibunda.
Naye mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Homera alipongeza uongozi wa chuo kikuu cha kilimo SUA kufanya maamuzi ya kuanzisha tawi katika wilaya ya Tunduru kwani fursa kubwa sana kwa mikoa ya kusini ambayo uchumi wao mkubwa ni kilimo.
Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wakionesha hati za makabidhiano ya majengo kwa ajili ya kuanza kutoa fursa mbalimbali za kufundisha katika Tawi jipya la Tunduru.wa kwanza kutoka kulia ni kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduru ndg Jonathan Albano Haule, wa pili ni Mwenyekiti wa Halmashauri MH.Mbwana Mkwanda Sudi, akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Zuberi Homera.
Mh. Homera aliendelea kusema wilaya ya Tunduru imepakana na hifadhi ya wanyamapori na pori la akiba hivyo kuanzishwa kwa tawi la chuo cha SUA kutasaidia kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ya namna bora ya kukabiliana na wanyama waharibifu mkoani Ruvuma.
Aidha mkuu wa wilaya aliomba kipaumbele cha kozi za kilimo kutolewa katika tawi la Tunduru ili kuendana na mahitaji ya wananchiwa Tunduru kwani kwa asilimia kubwa uchemi wao unategemea kilimo cha mazao lakini kuna upungufu mkubwa wa wataalam wa Kilimo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda wakishirikiana na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma zuberi Homera kufungua bango la Chuo Kikuu cha Sokoine Tawi la Tunduru baada ya kusaini Mkata wa makabidhiano ya majengo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Namwinyu Mh.Thabiti S.Thabiti akiongea kwa niaba ya wananchi alishukuru sana kwa uamuzi uliofanywa na serikali kupeleka chuo katika kata yake , lakini pia aliahidi kutoa ushirikiano wa kila hali katika kuhakikisha kuwa wanaanza ujenzi wa zahanati mara moja.
Mh.Thabiti S.Thabiti alisema wananchi wako tayari kutoa maeneo kwa ajili ya upanuzi wa eneo la chuo kikuu cha kilimo SUA ili kusogeza huduma ya elimu kwa wananchi wa Tunduru na wilaya jirani, alisema “hii ni fursa ambayo tumeisubiri kwa muda mrefu lakini sasa ipo kwetu kwani watu wa kusini tulisahaulika sana”
Wananchi wa kijiji cha Darajambili Kata ya Namwinyu wilayani Tunduru wakifuatilia kwa karibu maelekezzo ya mkuu wa wilaya katika hafla fupi ya makabidhiano ya Majnego kwa ajili ya kuanzishwa kwa kampasi ya tunduru ya chuo cha kilimo Sokoine.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.