Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima na wadau wa masoko ya mazao. Mfumo huu umesaidia kujenga uhusiano mzuri na wa haki kati ya mkulima na mnunuzi wa mazao. Kabla ya mfumo huu, kulikuwa na unyonyaji ambapo wakulima walikuwa wanauza mazao yao kwa bei ya chini sana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa kauli hii katika mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula Africa (AGRF 2023). Alisisitiza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa kiunganishi kizuri baina ya wakulima na soko, na umesaidia kuondoa unyonyaji uliokuwepo hapo awali.
Pichani ni Zao la Mbaazi
Mfumo huu umewaletea manufaa makubwa wakulima, hasa katika Wilaya ya Tunduru. Kwa msimu huu, mkulima wa ufuta ameweza kuuza kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo moja, na mkulima wa mbaazi ameweza kuuza si chini ya shilingi 1,500 kwa kilo moja. Hii ni bei nzuri na inawawezesha wakulima kupata faida kubwa zaidi.
Pichani ni Zao la Ufuta
Serikali chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Dkt.Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kuboresha miundombinu na mifumo ya kuwezesha mfumo huu wa stakabadhi ghalani. Hatua hizi ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kuna muunganiko mzuri baina ya mkulima na mnunuzi wa mazao. Hatua hizi zitawasaidia wakulima kupata masoko bora zaidi na kuondokana na unyonyaji.
Pichani ni Zao la Korosho
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa Wilaya zinazoongoza katika kilimo cha zao la Korosho,Ufuta na Mbaazi. Jitihada zake za kuboresha kilimo, kutoa Elimu kwa wakulima, kuimarisha masoko ya ndani na nje zimeleta mafanikio makubwa na kuleta maendeleo ya kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.