Na theresia mallya.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Chiza Cyprian Marando wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili (2) ya kutoa elimu ya mafunzo ya uelimishaji rika na stadi za maisha kwa vijana kutoka tarafa saba za wilaya ya Tunduru yaliyofanyika katika ukumbi wa klasta Tunduru mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 26 hadi 27.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi alisema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa na serikali imeamua kuwekeza kwa vijana kwani ndio kundi kubwa litakaloleta mabadiliko chanya kwa jamii katika mapinduzi ya uchumi wa viwanda.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Chiza Marando alisema katika risala iliyosomwa na muwezeshaji ngazi ya mkoa imeeleza wazi malengo ya mafunzo haya ya ueleimishaji rika kuwa ni kijana kujitambua yeye ni nani, anafanya nini na ni wapi anakokwenda na kuweza kupambana na changamoto za kimaisha zinazowakumba vijana wengi waliokata tamaa.
Ndg Marando aliendelea kutanabaisha kuwa halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika kutekeleza sera na miongozo ya serikali imetenga fungu kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu ya vijana ili kuongeza wigo wa ajira na kupunguza utegemezi, endapo vijana watafanya kazi zitakazowaingizia kipato hali ya uchumi wa kaya utabadilika na hata wa mtu mmoja mmoja.
Alisema “umri wa kijana ni kuanzia miaka 18 hadi 35 na huu ndio muda sahihi wa kuwekeza kwani ndio unakuwa na nguvu za kukuwezesha kufanya kazi za uzalishaji, hivyo niwaombe vijana wote mliofika katika semina hii musikilize kwa makini na kuyafanyia kazi mafunzo ya ujasiriamali mtakaofundishwa na wakufunzi”
Pia aliwakumbusha nidhamu ya matumizi ya fedha na kuwa na malengo kwa kile kidogo wanachopata ili kutengeneza maisha ya baadaye, kuepuka tamaa ya vitu ambayo haviko katika bajeti yako, kwani kijana ukiwa na tabia hiyo hutaweza kufikia malengo.
Ndg Chiza Marando alisema “tumewaita hapa kuwapa elimu itakayowasaidia, vijana mnatakiwa kujifundisha, mabinti msikubali kudanganywa na wanaume ni waongo sana,angalieni ndoto zenu fanyeni kazi msisubili vya kupewa”
Sambamba na hayo alizungumzia suala la Ukimwi ambalo ni janga la taifa na limekuwa likiwatesa sana vijaa wengi kutokana na kuijiingiza katika ngono zembe wakiwa na umri mdogo, aliwaasa vijana kuwa waaminifu kwa wenza wao ili kuondokana na adha na madhila katika familia nyingi.
Aliendelea kusema kuwa unapopata maambukizi ya vizuri vya ukimwi kutokana na ngono zembe au kuchepuka unasababisha matatizo kwa mwenza wako na familia yako kwa ujumla kwani watoto ndio wanataseka kwa starehe zako na ubinafsi wako.
Alimalizia kwa kuwataka vijana kujiunga kwenye vyama vya msingi vya ushirika, “huko mnapeleka korosho zenu na makato ya shilingi 30 ya kuendesha shughuli za chama unakatwa lakini wewe sio mwanachama hivyo ukijiunga unapata nafasi ya kuweza kutoa mchango wa mawazo na pia kugombea nafasi za uongozi” alisema ndg Chiza Marando.
Nao vijana walioshiriki mafunzo hayo walisema watakayojifunza wataenda kuyafanyia kazi na kuhakikisha kuwa wanajikwamua na hali ngumu za maisha kwa kujiongozea kipata na pia kuepekana na mila potovu zilizopo katika jamii yao, hivyo elimu hii tunatarajia kwenda kuitoa kwa vijana wenzetu ili iwe endelevu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.