WAZAZI TUWAFUNDISHE NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA MAADILI.
wazazi wameombwa kuwafundisha na kuwasimamua watoto wao katika maadili yaliyo mema , yametahadhalishwa hayo katika hotuba ya mgeni rasmi Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tunduru Adv. Julius S. Mtatiro katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika kata ya Ligunga Kijijji cha Ligunga ,iliyowasilishwa na mwakilishi wa mgeni rasmi makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mh. Saidi Bwanali .
Mhe.Bwanali aliwasihi wazazi kuwalea watoto wao katika misingi ya kidini na taratibu za kimungu ,aidha aliendelea kuwataka wazazi kudumisha na kuonesha upendo wa dhati kwa watoto wao.
Aidha amewataka viongozi kuonesha ushirikiano na mawasiliano yaliochanya pale ambapo wazazi wanahitaji msaada katika malezi ya watoto ,na kuisisiriza jamii kwa ujumla wake kutimiza wajibu wao katika malezi ya watoto hasa kwa nyakati hizi za digitali kwa kuwazuia watoto katika matumizi ya mitandao hasa katika mahudhui yasiofaa yanayooneshwa pia katika programu mbalimbali za televisheni.
alisema tuendelee kuwafundisha zile tabia na adabu ambazo tuliridhishwa toka kizazi cha nyuma ili kizazi kijacho kiwe chema kama vile kilivyokuwa toka hapo zamani.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.