Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Ruvuma Bwana. Saidi Juma Kijiji inaendesha zoezi la kliniki za ardhi katika Wilaya ya Tunduru.
Zoezi hili litaendelea kwa siku tatu, kuanzia tarehe 10 hadi 12 Oktoba 2023, lengo ni kutoa huduma kwa wananchi wa Tunduru, ikiwa ni pamoja na, kutoa hati ya papo kwa hapo kwa wananchi ambao wamekidhi vigezo, kusikiliza malalamiko ya ardhi na kutoa Ankara kwa wananchi wanaohitaji kupata hati na kupata kodi ya ardhi, na huduma nyingine za Ardhi kama utoaji wa mipango ya matumizi ya ardhi, utoaji wa vibali vya ujenzi, utoaji wa hati za udhamini na utoaji wa hati za uhamisho wa ardhi.
Akizunguza katika ufunguzi wa zoezi hilo ofisi za ardhi wilayani Tunduru, Bwana Saidi Juma Kijiji alisema kwamba, Serikali inahakikisha hati zinapatikana kwa urahisi zaidi, imeboresha mfumo wa usajili wa ardhi ili uweze kutoa hati haraka kwa wananchi wake. Vilevile,imepunguza gharama za umilikishwaji wa ardhi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
“Faida mojawapo za hati ni kupunguza migogoro na kuongeza usalama wa ardhi, kwakuwa itakuwa imepangwa na kupimwa,” Alisema “Wananchi wote waliopimiwa ardhi wafike ofisi za ardhi ili waweze kukamilisha taratibu za umilikishwaji na kupatiwa hati miliki”
Zoezi la kliniki za ardhi litasaidia kutoa huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru kwa uharaka zaidi. Hati ni mali, kwakuwa itampatia mwananchi uhakika wa umiliki wa ardhi yake, inaweza kusaidia katika kupata mikopo kutoka benki na taasisi nyingine za kifedha.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.