Katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji duniani Halmashauri ya wilaya ya Tunduru iliyopo katika mkoa wa Ruvuma wameungana na nchi nyingine zote duniani kufanya sikukuu hiyo katika Kijiji cha Amani ambapo mradi mkubwa wa maji wa Amni umekabidhiwa kwa wananchi wa vijiji vya Amani,Chiungo,Meamtwaro na Mchengamoto.
Akisoma risala ya utekelezaji wa mradi wa maji Amani kwa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Tunduru Ndg Eberhard Halla unaodhaminiwa na benki ya dunia alisema kuwa mradi wa maji Amani umegharimu jumla shilingi milioni 978,445,572.50. hadi kukamilika.
Alisema mradi huu wa maji Amani jumla ya vituo vya kutolea huduma ya maji 48 vimejengwa katika vijiji vya Amani 17, Chiungo 10, Meamtwaro 8, Mchengamoto 10 na kitongoji cha Mkarachani 3 ambapo mradi huu unatumia chanzo kimoja cha maji cha mto Nambango kilichpo Kijiji cha Amani.
Kaimu Afisa Utumishi wilaya Ndg John Mpangala akifanya utambusho wa viongozi katika maadhisho ya kilele cha wiki ya maji Duniani ambayo kiwilaya yamefanyika katika Tarafa ya Namasakata.
Akihutubia wananchi wa kata ya Namasakata katika kilele cha wiki ya maji duniani mgeni rasmi ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Mh Mbwana Mkwanda Sudi alisema kwanza mradi anaoukabidhi kwa wananchi wa vijiji vinne vya Chiungo, Amani, Mchengamoto na Meamtwaro ni miongni mwa miradi 10 katika vijiji kumi vya Tunduru inayofadhiliwa na benki ya dunia.
Mh.Mkwanda Sudi aliendelea kusema kuwa katika maadhimisho ya wiki ya maji duniani inayoanza tarehe 16 hadi kilele chake tarehe 22 machi kila mwaka shughuli zifuatazo hufanyika kutoa elimu ya uhamasishaji juu sera za maji nchini, elimu ya utunzaji wa mazingira na namna ya kutunza na kulinda vyanzo vya maji.
Aidha mwenyekiti aliwataka wananchi kuchangia mradi huo ili uwe endelevu na udumu kwani serikali imewekeza fedha nyingi sana katika mradi huu na maeneo mengi ya Wilaya ya Tunduru wanatamani kupata mradi kama huo, hivyo niwatake madiwani wa Kata ya Namasakata na Misechela ambao wanapata huduma ya maji kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kutunza, kuchangia na kulinda mradi huu.
Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Tunduru ndg Eberhad Halla akikabidhi Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji Amani uliogharimu Jumla ya shilingi milioni 978,445,572.50. hadi kukamilika, mradi huu umewafikia wananchi wa vijiji vinne vya Amani, Mchangamoto, Chiungo, Meamtwaro pamoja na kitongoji cha Mkarachani
Mwenyekiti alisema “ni nyema vijiji vikajiwekea utaratibu wa kuchangia huduma ya maji ili mradi uwe endelevu lakini kuna makundi maalum katika jamii ambayo sio lazima kuchangia mfano wazee na walemavu hawa inabidi kukadiriwa kiwango cha lita za maji wanazotumia kwa siku”
Vilevile aliwakumbusha wananchi juu ya suala zima la utunzaji wa mazingira na kulinda chanzo cha maji cha mto Nambango, ni vyema kujikinga na magonjwa mtambuka ambayo hayana tiba kama ukimwi na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira kama kipindupindu na malaria.
Wanakijiji wa kijiji cha Amani wakiwa katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji Duniani kilichofanyika katika Tarafa ya Namasakata wilayani Tunduru.
Alihitimisha kwa kutilia mkazo katika sula zima la wananchi kuthamini elimu kwani ndio urithi pekee watakaowaachia watoto wao, hivyo niwaagize wanafunzi wazazi na walezi kuacha tabia za kuwazua watoto wao kwenda shule na pia kuacha tabia za kuwahamasisha kufanya vibaya katika mitihani ya darasa la saba kwani elimu inatolewa bure, na azma ya serikali ni kuona kuwa watoto wote wanapata elimu bora.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.