SERIKALI YAKAMILISHA UKARABATI WA KISIMA CHA MAJI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MASONYA
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kupitia fedha za ruzuku ya maendeleo imefanya ukarabati wa kisima cha maji katika shula ya wasichana Masonya iliyopo Kata ya Masonya wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.
Ambapo katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2016/2017 imefanya ukarabati wa kisima hicho kwa kutumia tsh 2,000,000 ili kuhakikisha shule inapata huduma ya maji ya kutosha ili wanafunzi wapate muda wa kutosha kujisomea na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Masonya Bi Elice Banda anaishukuru serikali kwa kutatua changamoto ya maji katika shule ya wasichana Masonya.
Kisima cha kusukuma maji kwa mkono katika shule ya wasichana Masonya kilichokarabatiwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, katika picha ni Afisa Biashara Wilaya Ndg Anselim Mawazo akifanya majaribio ya kupandisha maji wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mardi huo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.