Baraza la Madiwani, Menejimenti na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wanapenda kukupongeza kwa dhati Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka mitatu tangu ulipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, tumeona maendeleo makubwa Wilayani Tunduru katika sekta mbalimbali. Tunashukuru sana kwa kuleta fedha nyingi zilizofanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa shule mpya, ukarabati wa Hospitali ya Wilaya na ujenzi wa Zahanati katika maeneo ya vijijini, na uimarishaji wa sekta ya kilimo ambacho ni uti wa mgongo, na kwa kuwa ni chanzo kikuu cha uchumi wa Wananchi wa Wilaya ya Tunduru. Miundombinu hii imeboresha kwa kiwango kikubwa sana maisha ya wananchi wa Tunduru na imeleta mabadiliko makubwa katika wilaya yetu.
Hospitali ya Wilaya ya Tunduru iliyofanyiwa ukarabati na Serikali ya awamu ya sita, inaendelea kutoa huduma zake kikamilifu.
Pichani: Muonekano wa moja kati ya Shule za Msingi Mpya zilizojengwa kupitia mradi wa Boost, mradi huu umetekelezwa ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya sita.
Tunathamini sana uongozi wako thabiti na dhamira yako ya dhati ya kuleta maendeleo kwa Watanzania wote. Tunaamini uongozi wako utaendelea kuleta mafanikio makubwa zaidi kwa taifa letu katika miaka ijayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inafurahi sana kuungana na Watanzania wote katika kusherehekea mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wako bora.
Tunakutakia kila la kheri katika kuendelea kutekeleza majukumu yako mazito ya kuongoza taifa letu. Tunakuhakikishia ushirikiano kamili katika kuunga mkono juhudi zako za kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.
Mungu ibariki Tanzania.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.