Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma dk Bilinith S Mahenge katika mkutano wa hadhara aliyofanya na wananchi wa tarafa ya Matengama katika kata za Jakika na Kalulu ambazo zimeathiriwa kwa kiasi kikibwa na wanyama waharibifu wanaovamia makazi ya wananchi na kusababisha mauji na uharibufu wa mazao mashambani.
Aidha alisema serikali inamthamini binadamu kuliko wanyama na binadamu ndio wenye utashi na wamepewa mamlaka ya kutawala na viumbe vyote na kutawala mazingira hivyo binadamu ni muhimu sana "niwaombe wananchi mtambue kuwa serikali inawathamini sana binadamu kuliko wanyama na niawaombe mufute kauli ya kuwa serikali inathamani tembo kuliko maisha yenu" alisema Dk Mahenge.
aliendelea kusema kuwa serikali inafanya kazi mchana na usiku kuleta maendeleo kwa wananchi wake na anaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi ili kutekeleza wajibu wao kwa wananchi katika hali ya utulivu na amani na yapo majukumu ambayo serikali inatakiwa kuyatekeleza kwa wananchi lakini kuna sehemu nyingine ambayo ni kya wananchi kutekeleza hivyo ni vyema kila mtu akafanya kwa sehemu yake ili kuchochea maendeleo.
Mkuu wa Mkoa aliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa vijiji ambao sio waaminifu na wamefikisha halmashauri ya wilaya ya Tunduru na Mkoa wa Ruvuma katika hali mbaya kwa kuhalalisha makundi makubwa ya mifugo kuingia katika hifadhi za taifa, mapori ya Akiba na Misitu ya Hifadhi ya Jamii hali inayosababisha wanyamapori hususani Tembo kuhama katika makazi yake na kuvamia makazi ya wananchi na kuleta madhara makubwa ya uharibifu wa mashamba ya wakulima na mauji ya raia.
alisema mpaka kufikia agosti 30 mwaka 2017 jumla ya vifo
serikali imeona uharibifu huo na imepanga mipango mikakati ya kuweza kulimaliza tatizo la wanyama waharibifu kutoka katika taasisi zinazosimamia wanyamapori ndani ya wilaya ya tunduru kwa kushirikiana na serikali, wadau kutoka vokosi vya PAMS Foundation, KDU kanda ya Kusini, WWF kanda ya kusini, wahifadhi pori la akiba seleous, Jumuiya za Nalika na Chingoli pamoja na askari wanyama pori Halmashauri.
Askari wanyama pori katika kambi ya pori la akiba la selous kanda ya kusini wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma DK binilith S Mahenge wakati wa ziara ya kamati ya ulinzi na usalama Mkoa na wilaya ya Tunduru, na wadau wa uhifadhi wa wanyamapori waliopo wilayani Tunduru ya kupanga mikakati ya kuwakabili wanyama waharibifu hususani Tembo na fisi katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.