Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Bibi Christina Mndema , amefanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 8 hadi 9/8/2018 Wilayani Tunduru ya kukagua hali ya Usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji katika vituo vya mpakani vya Makande na Wenje.
Katika ukaguzi huo,Mhe.Mndeme amesema ardhi ya Tanzania pamoja na maliasili nyingine za Taifa zetu zinatakiwa kulindwa kwa hali na mali ili kuhakikisha zinakuwa na manufaa kwa wananchi na Uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka watendaji na wananchi waliopo katika vijiji vyote vya mpakani kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na kuwakumbusha kuwa mpaka huu ni wa kihistoria kwa sababu umechangia kupatikana kwa uhuru wa Nchi ya Msumbiji.
Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa na wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bi.Christina Mndeme wakiwa katika ukaguzi wa mpaka wa Tanzania na Msumbiji maeneo ya Wenje na Makande
Pia ameagiza masuala ya Ulinzi na Usalama wa mpaka huu yawe ni agenda ya kudumu katika vikao vya vijiji ambavyo vitasaidia kuwatambua wageni ambao wanaingia nchini bila kufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vibali vya kusafiria kuingia nchini.
Hata hivyo Bibi Mndeme aliwataka wananchi kutoa taarifa za viashiria vinavyoweza kuvunja amani katika maeneo yao inapojitokeza.
"Nchi yangu Usalama Wangu"
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.