Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Tunduru uliofanyika katika viwanja vya baraza la Idd Tunduru mjini wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Alisema hakuna kubughudhiwa kwa mfanyabiashara mwenye kitambulisho kwani atakua ameshalipa ushukuru kwa kuchukua kitambulisho kitachotumika kwa kipindi cha mwaka mmoja,ambacho anachangia shilingi elfu 20,000. "Nia ya serikali kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo kuongeza ufanisi katika mitaji na kuwa wafanyabiashara wa
Kati au wakubwa sababu ukaguzi utafanyika baada ya mwaka mmoja ili kuona mafanikio yaliyojitokeza"
RC mndeme alitaja wafanyabiashara ambao watapewa vitambulisho ni pamoja na bodaboda,waendesha bajaji, mama lishe,wamiliki wa nyumba,wachoma wanyama,wamiliki wa magenge,wachimbaji wamadini,wapaka kucha rangi,wasajili wa laini za simu,wamiliki wa magenge nyumbani,wauza kakuta,mihogona mtu peyote anayefanya miamala ya fedha mzima awe na kitambulisho na kwa wale wenye mtaji zaidi ya milioni nne ambao wana leseni za Mamlaka ya mapato Tanzania.
Alisema kama ndani ya familia baba na mama ni wafanyabiashara kila mmoja achukue kitambulisho chake lakini kila mkuu wa Idara apangiwe Kata ya kusimamia ili kuongeza ufanisi na kuleta uhalali wa kuzua baadhi ya watu ambao wanaingia mtaani kulaghai wananchi.
Hata hivyo zoezi mwisho wake ni tarehe 28 February 2019 na halmashauri ya Tunduru ina vitambulisho elfu 10,000 ambavyo vinatakiwa kuwafikia walengwa kwa makati ili kutekeleza kwa wakati azuma ya serikali ya swami ya tano ya kuwasaidia wanyonge na inafika mpaka ngazi ya kitongoji.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.