Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Kanali Laban Thomas amewataka Wananchi wa Wilaya ya Tunduru washiriki Kikamilifu katika zoezi la Sensa ambapo Kitaifa litafanyika tarehe 23/08/2022 uku akiwataka viongozi wa Ngazi mbalimbali kila mmoja ashiriki kuhamasisha Zoezi la Sensa Sambamaba na hayo RC –Kanali Laban aliwashukuru Wabunge kwa jitihada zao wanazo zionyesha katika kuhakikisha zoezi la Sensa Tunduru linafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.
Rc – Laban aliendelea kutolea ufafanuzi wa Changamoto ya Wanyama pori Waharibifu aina ya Tembo ambapo alisema”Ofisi yake kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii wamejipanga kuongeza idadi ya Askari ya Wanyama pori ambao kwa uwepo wao kwa wingi itaongeza nguvu kazi kuliko kama sasa idadi ya askari ni chache sana na maeneo yanayo vamiwa na tembo ni mengi sana uwepo wa askari hao utasaidia kufika kwa wakati pale Tembo wanapo vamia mashamba na makazi ya watu”.
Kuusu swala la Mifugo holela Rc – Laban alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ndg Julius Mtatiro aendelee na hatua ambazo alianza nazo uku hakikishe kila mfugaji aelekee kwenye kitaru ambacho alipangiwa na kama Mfugaji atakuwa hana kitaru hatua kali zichukuliwe zidi yake lengo kila Mwananchi aishi kwa kufuata sheria ya Nchi.
Mwisho Rc – Laban aliwashukuru Wananchi wote wa Jakika kwa kujitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza mambo ambayo alipanga kuwaambia uku akiwaomba wayafanyie kazi yale ambayo wamejadiliana ikiwemo zoezi kubwa la Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika 23/08/2022 ambapo itakuwa siku ya Mapumziko kwa Nchi Nzima .
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.