Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme ameuopongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya Tunduru kupata hati safi katika ukaguzi uliofanywa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali mwaka wa fedha 2017/2018 ikiwa ni matokeo ya utendaji kazi mzuri na ushirikiano wa wataalamu, madiwani na wabunge.
Akiwa katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Tunduru la kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 alisema mwenendo wa Halmashauri ni mzuri kwa kuangalia miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2014 hadi 2018, Halmashauri ya Tunduru imekuwa ikipata hati safi kwa kipindi cha miaka 3 mfulululizo, isipokuwa mwaka 2014/2015 ndio ilipata hata yenye mashaka.
Alisema ni vizuri Halmashauri ikaweka mpango mkakati wa kudhibiti na utunzaji wa nyaraka katika kuhakikisha kuwa wakati wa ukaguzi nyaraka zote muhimu zinakuwepo na kupewa wakaguzi.
Alisema sababu za kuwa na hoja nyingi za nyuma ambazo hazijafungwa katika Halmashauri ni ushiriki mdogo wa wakuu wa idara katika kuaandaa majibu ya hoja, kukosekana kwa ushirikiano wakati wa ukaguzi kwa wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa ukaguzi wa hoja za serikali.
Mkuu wa mkoa huyo alikemea tabia ya baadhi wa watumishi wanaokusanya mapato kwa kutumia mashine za POS kuchelewa kupeleka fedha benki kuchukuliwa hatua haraka sababu wanahujumu Halmashauri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Mh.Mbwana Mkwanda Sudi alisema kuwa usimamizi utafanyika katika utunzaji wa kumbukumbu ili kuepuka hoja ambazo sio za msingi katika halmashauri
Aidha Mh. Mbwana Mkwanda Sudi alisema Halmashauri imekumbana na changamoto ya kuchangia kidogo mfuko wa wananwake, vijana na walemavu ambapo halmashauri imetoa asilimia 28 ikiwa ni kutokana na halmashauri kuwa na chanzo kimoja kikubwa cha mapato ya ndani yatokanayo na zao la korosho hivyo kukosekana na fedha hizo kumekwamisha utekelezaji wa bajeti.
Naye mkaguzi wa hesabu za serikali mkoa wa Ruvuma aliipongeza halmsahuri kupata hati safi lakini alizitaka idara zenye hoja kuwasilisha vielelezo ili hoja zilizopo ziweze kufungwa na kutoa ushirikiano wa karibu kwa wakaguzi ili kuepuka kuzalisha hoja Zaidi.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.