Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa katika Hospitali ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma ikiwa ni moja ya Lengo la Benki hiyo kurejesha faida kwa jamii na kuifikia jamii katika mahitaji yao muhimu.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivo Kaimu Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kusini Ndg. Romani Degeleki amesema kama ilivyo desturi, benki ya Nmb inarudisha kwa jamii asilimia ya faida katika shughuli zinazofanywa na Benki ya NMB.
“tunafanya biashara na jamii kwahiyo kwenye faida ambayo tunaitengeneza kila mwaka tunatenga kiasi cha kuweza kurudisha kwa jamii yetu” Alisema
Vifaa ambavyo vimekabidhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru ni Mashuka 150, Vitanda 10, Magodoro 10, Viti vyenye Magurudumu (Wheel chair) 04, Vitenga Wodi (screen cutting) 08 ambavyo kwa ujumla vina gharimu Zaidi ya shilingi milioni 10.
Akikabidhiwa vifaa hivyo mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Wakili ,Julius S.Mtatiro ameishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo wa vifaa katika hospitali ya wilaya kwani itakuwa ni moja ya kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita, pia amewataka watendaji hasa wanaokabidhiwa vifaa hivyo kutambua majukumu yao na kuweza kuvitunza vifaa hivyo.
Aidha Mhe.Mtatiro ameiomba Benki ya NMB kuendelea kuunga mkono maendeleo ya wilaya ya Tunduru kwa kuzidi kutanua msaada katika sekta nyingine muhimu kama elimu, na kuwataka kusogeza huduma zao za kifedha hasa maeneo ya vijijini.
“Kitendo mlichokifanya sio tu mmelejesha kwa jamii,bali ni shughuli ya kurejesha kwa mwenyezi mungu, Alisema “kitendo hiki ni kikubwa sana katika wilaya yetu kinaenda kuongeza tija katika sekta ya Afya”.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi Mtendaji Ndg. Masanja Kengese ametoa shukrani zake za dhati kwa Benki ya NMB kwa kuunga mkono Maendeleo ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia ametoa rai kwa taasisi zingine kuiga jitihada hizi za kusaidia jamii.
Kwa niaba ya Hospitali ya wilaya ya Tunduru Daktari Wilfred Rwechungula Mganga Mkuu (W) Tunduru ametoa shukurani zake za dhati kwa benki ya NMB kwani vifaa hivi vinaenda kusaidia moja kwa moja wananchi wa Wilaya ya Tunduru, na kuomba kuzidi kuweka kipaumbele katika huduma za Afya.
Benki ya NMB imekuwa ni miongoni mwa benki ambayo inasaidia jamii katika Nyanja za Afya, Elimu na Mazingira na kuweza kuwasogezea wananchi huduma karibu Zaidi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.