MSIBWETEKE KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI LENGO NIKUFIKIA 100%
Imewekwa : October 20th, 2024
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amepongeza uongozi wa Wilaya ya Tunduru kwa ujumla kwa kuweza kufanya kazi nzuri ya hamasa ya kuandikisha wananchi katika orodha ya wapiga kura na maandalizi mazuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujumla.
Kanali Abbas amesema Mkoa wa Ruvuma umetangazwa kama ni Mkoa wa pili katika uandikishaji wa wapiga Kura ikiwa iko nyuma ya Mkoa wa Tanga, lakini niendelee kusisitiza takwimu hizi zisitufanye tukabweteka kwani siku zimebaki chache hivyo tuongeze juhudi na mikakati kufikia asilimia mia moja. Aidha Taarifa hii ameitoa 17 Octoba,2024 katika ukumbi wa SKYWAY mjini Tunduru.
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndugu.Chiza Marando alitoa maelezo ya muenendo wa hali ya uandikishaji wapiga Kura wapatao 243,364 kati yao wanaume ni 117,199 na wanawake 126,165. Alisema Marando hadi kufikia tarehe 16 Oktoba 2024 Jumla ya walioandikishwa ni 131,042 kati yao wanaume ni 62,104 na wanawake ni 68,938 sawa na 53.8%.