MPANGO WA MSITU SHIRIKISHI KWA MANUFAA YA WANANCHI.
TUNDURU
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Tunduru limepitisha mpango wa usimamizi shirikishi msitu pamoja na sheria ndogo za kijiji cha Ngapa, katika mkutano wa Robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2016/2917 uliofanyika katika ukumbi wa klasta uliopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Akitoa taarifa ya mpango huo katika kikao cha baraza la madiwani Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg Abdallah H Mussa alisema kijiji cha Ngapa ni miongoni mwa Vijiji saba (07) vilivyoko kwenye usimamizi shirikishi wa misitu wilaya ya Tunduru.
alisema “mradi huu utavipa vijiji hivyo kumiliki misitu yao na kuingiza mapato katika vijijiji ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na lengo kuu ni ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu”
aidha mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu umefadhiliwa na shirika la WWF, na kufanya kazi pamoja na Shirika la MIPANGO, na MJUMITA katika utekelezaji wake.
Ndg Abdallah mussa aliendelea kusema kuwa katika Halmashauri ya wilaya mpaka sasa ina jumla ya vijiji sita 06 ambavyo ni Machemba, Sauti moja, Namakambale, Mindu, Songambele,na Msinji hivyo kwa kupitisha kijiji cha Ngapa basi Halmashauri itakuwa imeingia mkataba na WWF wa vijiji saba 07.
Hata hivyo aliendelea kusema kuwa mapato yatokanayo na mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu una faida kwa vijiji kutokana na asilimia 90 ya mapato yataelekezwa katika kijiji kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za maendeleo ya kijiji pamoja na asilimia kumi itapelekwa katika serikali ya Halmashauri.
Naye diwani wa Kata ya Ngapa Mh Said Ally Pindu alisema wananchi watafaidika sana na msitu huo na kuongeza mapato ya kijiji husika hivyo kuchochea maendeleo ya kata kwa sababu mapato yatakayopatikana asilimia 90 yatapelekwa katika miradi ya maendeleo ya kijiji.
Hata hivyo utunzaji wa misitu na usimamizi shirikishi wa wanakijiji katika utaboresha utunzaji wa mazingira na kutunza vyanzo vya maji hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuondoa tatizo la maji kwa wananchi.
Theresia mallya.
Afisa Habari (w)
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.