Bweni la wanafunzi wavulana katika shule ya sekondari Nandembo limeungua moto na kuteketea kwa Mali zote za wanafunzi zilizokuwamo, wakati wanafunzi wakiwa katika nyumba ya ibada.
Akiyoa taarifa ya moto kaimu afisa Elimu Wilaya Mwalimu Habiba mfaume alisema taarifa za kuzuka kwa moto walizipata majira ya saa moja na nusu jioni kutoka kwa uongozi Wa shule ya sekondari Nandembo za kutokea kwa moto na kuunguza bweni la wavulana.
Ukosefu Wa kikosi cha Zima moto katika wilaya ya Tunduru umesababisha mali za wanafunzi kuteketea kwa ni walitumia tu njia za asili kama mchanga na mitungu ya gesi ya Fire extinguisher iliyopo katika maeneo ya hostel kwa kushirikiana na majirani Wa shule.
Alisema bweni hilo walikua wanakaa wanafunzi 72 ambao vitu vyao vimeteketea kwa moto na ikiwa ni pamoja na magodoro, vitanda, madaftari na vifaa vingine vyote vilivyokuwamo ndani ya bweni hilo.
"Bweni hili walikua wanakaa wavulana Wa kidato cha pili, NNE na kwanza ambao vifaa vyao vimeungua ni baadhi ya vitu vichache vilivyoweza kuokolewa lakini asilimia tisini vimeungua moto"
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa lakini tunamshukuru mungu hakuna mwanafunzi aliyeumia au kupata madhara katika ajali hiyo ya moto.
Aidha Halmashauri ikiongozwa na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, mwenyekiti Wa Halmashauri na wakuu Wa idara walifika katika shule ya sekondari kukutana na uongozi Wa shule Nandembo kutoa pole lakini pia kuona njia za haraka watakazotumia kutatua tatizo hili.
Hatua za awali zilizochukuliwa na serikali ni kuonana na uongozi mzima Wa shule na kuandaa mikakati ya kuwafariji wanafunzi na walimu waliokumbwa na janga la moto lakini pia kuandaa njia za kuwasaidia wanafunzi wale Wa kidato cha NNE ambao wanatarijia kuanza mitihani yao mwisho Wa mwezi Octoba.
Kutafuta sehemu ya muda ambako wavulana ambao bweni lao vimeungua watakua wanakaa kwa muda wakati serikali ikijiandaa kuona namna watakavyojenga bweni jingine kwa ajili ya wavulana.
Walimu na wanafunzi Wa madarasa mengine walitakiwa kuwasaidia wenzao waliounguliwa na madaftari yao kutoa kopi ili waweze kujiandaa na mitihani iliyopo mbele yao.
" ni vizuri katika kipindi hiki walimu kuwasaidia wanafunzi Wa kidato cha NNE waliounguliwa na madaftari kuwasaidia kutoa kopi ya madaftari katika shule jirani za Tunduru sekondari, Mataka na Frenkweston ambao wana machine za kupiga kopi" alisema Mwalimu Habiba.
Aidha alimalizia kwa kusema kuwa serikali itafanya tathimini ya madhara yaliyojitokeza na muandisi majenzi pamoja na Fundi umeme wameagizwa, na uongozi Wa wilaya utafika katika shule ya sekondari Nandembo Siku ya ijumaa baada ya Tathimini kufanyika.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.