Leo tarehe 24/11/2022 umefanyika mnada wa tatu wa korosho katika wilaya ya tunduru kijiji cha kidodoma kwa kuuza kilo 2,345,129 za korosho zilizopo katika maghara sita yaliyopo katika wilaya ya Tunduru, wanunuzi nane (8) walijitokeza kutoa zabuni zao za kununua korosho hizo.
Baada ya kamati kuchakata bei za wanunuzi wote ,wanunuzi wawili(2) walionekana kuwa na bei ya juu kununua korosho zilizopo sokoni kwa siku ya leo ambazo ni:-
Kwa muktadha huo bei ya juu kuw 1,822 Tzs na bei ya chini kuwa 1,820 Tzs na kufanya bei ya wastani kuwa 1,821.07 Tzs bei ambayo wakulima waliridhia kuuza korosho hizo.
Pia katika mnada huo mwenyekiti wa chama cha ushirika ndg Mussa manjaula amewataka wakulima wa kidodoma walime mazao mbadala ili kuweza kukinga njaa na pia kujiongezea kipato chao kuliko kutegemea Zaidi zao la korosho ,na kuwasihi kuwahi furasa iliyotolewa na serikali ya mbolea za ruzuku na vifaa vya kufanyia kazi kama vile bomba za umwagiliaji dawa
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.