Mnada wa tano wa zao la Mbaazi umefanyika tarehe 28.09.2023 katika kijiji cha Tulieni, AMCOS ya Namitili Wilayani Tunduru, mnada huu utakuwa ndio wa mwisho kwa zao la Mbaazi msimu huu.
Katika mnada huo, jumla ya tani 302 za Mbaazi ziliuzwa. Kampuni saba zilijitokeza kununua Mbaazi hizo, na kampuni mbili zilishindanishwa kwa bei ya juu. Bei ya wastani ya Mbaazi hizo ilikua ni shilingi 1905.66 kwa kilo moja.
Akizungumza katika mnada huo Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika (TAMCU), Mussa Manjaule, amepongeza wakulima kwa kuuza mazao yao kwa bei nzuri. Pia amewahimiza wakulima kutanua mashamba yao ili msimu ujao kuwepo na mazao ya kutosha.
“Msimu huu tumepata mafanikio makubwa katika uuzaji wa zao la Mbaazi, hii ni kutokana na juhudi za Serikali pamoja na ninyi Wakulima wenyewe. Bei hii ni ya kuridhisha itawasaidia sana kuboresha maisha yenu”, alisema Manjaule. “Nawaomba mkatanue mashamba yenu ili msimu ujao kuwepo na mazao ya kutosha”.
Manjaule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Daktari, Samia Suluhu Hassan, kwa kutafuta soko zuri na uhakika la mazao mchanganyiko kwa ajili ya wakulima. Pia, amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mh. Wakili, Julius S. Mtatiro kwa juhudi zake katika kuhimiza Stabadhi Ghalani kwa wakulima.
Tunduru ni kati ya Wilaya zinazozalisha mazao mchanganyiko yanayouzwa kwa Stakabadhi ghalani ikiwemo na Korosho, ambapo kwasasa wakulima wapo kwenye maaandalizi ya msimu wa uvunaji Korosho kwa msimu wa 2023/2024.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.