Katika mnada wa kwanza wa korosho katika wilaya ya Tunduru Tarafa ya Nakapanya , mkuu wa wilaya Mh Julius Mtatiro alisisitza wakulima kuendelea kulima zao la korosho kwa wingi.
Pia alisisitiza wakulima kulima mazoa mengine ambayo yatawasaidia kukinga njaa na sio kujikita Zaidi katika mazao ya biashara ,na kuwapa taarifa wananchi kwamba Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ipo kwenye mkakati wa kushughulika na wanyama waaribifu wa mazao kama tembo kwa kuanzisha kituo cha askari wanyama pori ili kuthibiti tatizo hilo.
Pia alizungumzia suala la mbolea ya ruzuku ambayo itauzwa kwa bei pungufu ili kufanya shughuli za kilimo kuwa na tija katika uchumi wetu wa taifa la Tanzania na kumshukuru Mh Samia Suluhu Hassani kwa jitihada hizi za kuwawezesha wakulima kupata mbolea hizo kwa bei pungufu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.