DC HOMERA Amedhishwa na mwenendo wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia Korosho linalojengwa na serikali kwa udhamini wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kwa shilingi Bilioni 5.7
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera aliyasema hayo alipoafanya ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa kwa na kampuni ya wazawa ya Skycity ya jijini Dar es salaam Tanzania.
Mkuu wa wilaya Juma Homera aliendelea kuwapongeza wakandarasi na kuwataka wamalize ujenzi wa mradi huo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa kati ya CBT na mkandarasi huyo ili ghala hilo liweze kutumika kuhifadhi korosho za wananchi wa Tunduru.
Alisema “Ghala hili lina urefu wa mita 135 na upana mita 35 na linatarajia kuwa na uwezo wa kuhifadhi korosho Tan 15,000 mpaka 20,000 kwa wakati mmoja ghala hili mpaka kukamilka kwake litagharimu fedha za Kitanzania shilingi Billion 5.7”
Akieleza faida za ujenzi wa ghala hilo katika wilaya ya tunduru mkuu wa wilaya alisema kwamba kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa ghala hilo kutapunguza changamoto ya wizi wa rejareja wa korosho za wakulima kabla ya kufikishwa kwenye ghala kuu kwa ajili ya Mnada, pili kutawawezesha wakulima kuwahi soko lenye bei nzuri kwakuwa korosho zao zitawahi kuondolewa shambani na kufikishwa ghala kuu.
Mh.Homera aliwaomba uongozi wa bodi ya Korosho (CBT) kupitia kaimu mkurugenzi mkuu Prof Wakuru Magigi kufanya usimamizi wa karibu kwa mkandarasi anayetekeleza mradi huo ukamilike kwa wakati.
imetolewa na
Theresia Mallya
Afisa Habari halmashauri
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.