Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kanali Ahmed Abbas Ahmed afanya ziara Wilaya ya Tunduru na kufanya vikao vitatu kwa Viongozi wa Chama na Serikali ambao waliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe.Simon Chacha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Kikao cha Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,Wakuu wa Taasisi mbalimbali,Viongozi wa dini,Wazee maarufu, Viongozi wa vyama vya siasa,Waheshimiwa madiwani pamoja na wawakilishi wa wafanyabiashara na baadae mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Tunduru.
Katika mkutano aliofanya na Wananchi, Mhe. Kanali Ahmed alitoa nafasi kwa wananchi kuzisema kero zao ambazo nyingi zilitolewa ufafanuzi na yeye mwenyewe akishirikiana na wataalamu toka ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, pamoja na wakuu wa taasisi kama vile TANESCO, na TANROADS.
Aidha, Mhe. Kanali Ahmed alitoa taarifa ya uwepo wa Tamasha la 3 la taifa la Utamaduni ambalo litafanyika Mkoani Ruvuma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa,Dkt.Samia Suluhu Hassan, ambaye baada ya uzinduzi atafanya ziara katika Mkoa wa Ruvuma ikiwemo Wilaya ya Tunduru.
Na mwisho, Mhe.Mkuu wa Mkoa aliwashukuru Wananchi kwa mahudhurio na michango yao ya hoja huku akiwasisitiza kuwa na subra na uvumilivu wakati wa kupambana kuziondoa changamoto,ushirikiano baina ya viongozi wa serikali,Chama na Wananchi kwakuwa maendeleo na utatuzi wa changamoto Suluhu yake ni kufanya kazi kwa pamoja.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.