Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru (aliesimama) Mh Hairu hemed musa alimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MAMA SAMIA SULUHU HASSAN Kwa kuonyesha lengo la dhati la kuinua Elimu Nchini katupatia Milioni 200 kwajili ya Ujenzi wa Madarasa 10 Mapya Elimu Sekondari,
Pia katika mwaka wa Fedha 2021/2022 Serikali ya awamu ya sita imetoa jumla ya Bilioni 3.9 zilizo tumika kujenga Barabara za Lami Kilomita 3.16 kwa jumla ya Tshs 1,494,644,000.00, Barabara kwa kiwango cha Changarawe Kilomita 80 zenye jumla ya Tshs 1,280,000,000.00.
Pia Ujenzi wa daraja moja kubwa na madaraja madogo mawili ambapo jumla ya Milioni 400 zimetumia Aidha Wanatunduru tunatambua mchango wa Mama katika jitiada zake za kuhakikisha Tunduru tunapata Maji safi na salama Ndugu zangu sisi sote hapa ni mashuuda kwa Sasa kuna miradi mbalimbali ya RUWASA inaendelea kutekelezwa katika maeneo yetu ya kiutawala ikiwemo mradi mkubwa wa Maji wa Marumba kwenda Mchoteka, Upande wa Afya Ujenzi wa Vituo vya Afya vinne (4) ambavyo ni Masonya, Nalasi, Mchesi na Nampungu uliogharimu zaidi ya Bilioni 1.5 Unaendelea vizuri
Pia Mwenyekiti alipenda kuwashukuru Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu kwa Ushirikiano na Michango mbalimbali mnayoendelea kunipatia. Hii yote ni kwajili ya kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Tunduru Wanapata huduma bora na zenye tija.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.