Katika mkutano huo wa baraza madiwani walipata kusikiliza na kujua maendeleo ya miradi mbalimbali katika wilaya ya tunduru na kuweza kuhoji kwa kile kilichokuwa akijakaa sawa na kupata ufafanuzi.
Mkuu wa wilaya Ndg JULIUS NINGU katika mkutano wa baraza na madiwani wa wilaya ya tunduru kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya tunduru, mkuu wa wilaya alizungumzia mambo mbalimbali katika kikao hicho cha baraza pamoja na Ugonjwa wa uviko 19 tuweze kujikinga na ugonjwa huo, hali ya usalama katika wilaya ya tunduru , kuhusiana na kilimo mkakati katika wilaya ya tunduru hasa katika zao la mbaazi pamoja na sharia zizohusu mifugo katika wilaya ya tunduru ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji pia alizungumzia kuhusu na mapokezi ya mwenge katika wilaya ya tunduru mnamo tarehe 2/9/2021 ,na kuwataka madiwani kukamilisha miradi mbalimbali katika wilaya ya Tunduru.
Pia katika mkutano wa baraza la madiwani meneja wa tanesco wilaya ya tunduru alitoa ufafanuzi kuhusiana na bei ya uwekaji wa umeme kwa wateja wao .
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.