Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imefanya mkutano maalumu wa kufunga hesabu za fedha kwa mwaka 2022/2023, kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa inayozitaka Halmashauri nchini kufunga hesabu na kuwasilisha kwa mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh. Hairu Mussa alisema, Halmashauri ilikusanya kutoka vyanzo vyake (own source) zaid ya shilingi bilioni 4.3 ambayo ni sawa na asilimia 93 ya makisio ya mwaka shilingi bilioni 4.7.
Kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo, rasilimali za muda mrefu na mfupi za Halmashauri zimepanda thamani toka zaidi ya shilingi milioni 65 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia zaidi ya shilingi milioni 70 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
“Mapato tunayokusanya tunahakikisha ,yanaenda katika atekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ya kata na vijiji kuboresha huduma za jamii”
Akifafanua taarifa hiyo, ndugu Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Tunduru ndugu Masanja Kengese, amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha shilingi bilioni 4.8.
“Rai yangu kwa waheshimiwa madiwani kuweza kushirikiana na halmashauri katika kudhibiti mapato, ukizingatia mapato ya halmashauri ya wilaya ya Tunduru yanapatikana kupitia mazao, hivyo, tunawaomba waheshimiwa madiwani kusaidia kudhibiti utoroshaji wa mazao”. Alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani Said Kiosa(kata ya Nanjoka) na Daudi Amlima (kata ya Nakayaya) wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Wilaya ya Tunduru.
Halmahauri ya wilaya ya Tunduru ina Tarafa 7 ,kata 39 ,vijiji 157 na vitongoji 1179 ,Serikali ya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inahakikisha maeneo yote yanafikiwa na huduma za jamii kupitia mapato ya ndani na mapato kutoka Serikali kuu.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
28/08/2023.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.