Mafunzo ya tusome pamoja ni mradi unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID) unaolenga kusaidia kuboresha stadi za za kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) katika shule za awali na madarasa ya chini ya shule za msing (1-4) katika mikoa minne ya Tanzania bara (Ruvuma, Mororgoro,Mtwara,Iringa) pamoja na shule zote za serikali zanzibar.
USAID Tusome pamoja kwa kushirikiana na serikali walitoa mafunzo mkoa wa Ruvuma ya mpango Jamii wa uhamasishaji na utekelezaji Elimu (MJUUE) wenye lengo la kuhamasisha jamii katika kubaini changamoto katika sekta ya elimu msingi zinazoathiri ubora wa elimu na ufaulu. Pia kuisaidia jamii ishiriki katika kuandaa mipango ya elimu kwa ajili ya watoto wao hivyo kuimarisha ushiriki wa jamii katika kuboresha utoaji elimu.
Mratibu wa mafunzo hayo ya USAID Tusome pamoja alisema kuwa walitoa mafunzo ya siku tatu ya wawezeshaji jamii Elimu 1,400 kutoka shule 770 za msingi za serikali mkoani Ruvuma ambao pamoja namambo mengine wameweza kusaidia kuongoza uaandaaji wa wa dira na mipango kazi ya muda mfupi ya shule za msingi na mipango hiyo kuridhiwa na jamii, wahamasishaji watafanya kazi kwa kujitolea kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli zote zinazohusu elimu katika shule zao.
vile vile leo tarehe 05/10/2017 ni muendelezo wa mafunzo waliyopata awali na watatoa mrejesho wa shughuli walizofanya katika maeneo yao katika kuandaa mipango kazi ya muda mfupi ya shule za msingi na mipango hiyo kuridhiwa na jamii.
Akizungumza na wahamasishaji kutoka katika kata za wilaya ya tunduru kaimu mkurugenzi mtendaji (W) mwalimu George Mbesigwe ambaye ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu aliyemuwakilisha mkurugenzi mtandaji alisema mafunzo haya yamefanyika kwa awamu ya pili na yale ya awamu ya kwanza yalienda vizuri kwani wameandaa mpango lakini utekelezaji umeanza kufanyika kwani kuna baadhi ya shule ambazo zimeanza tayari kujenga matundu ya choo.
"nimepita katika shule ya msingi mjimwema nimekuta wanafyatua Tofali kwa ajili ya kuongeza matundu ya vyoo ni namna gani mafunzo haya yana mrejesho chanya kwa jamii na kuleta mabadiliko"
Alisema pamoja na serikali na wadau wa maendeleo kuwezesha mradi wa uaandaji wa mipango lakini kumbukeni kuwa shule ni mali ya jamii na huo ni wajibu wa kila mtu kujua hilo na tunapotekeleza miradi yetu katika maeneo yetu tujue kuwa tunafanya kwa ajili yetu na sio kwa ajili ya serikali.
pia niwakumbushe lengo la mradi wa tusome pamoja unaofadhiliwa na shirika la maendelo la kimataifa la watu wa marekani kuleta hamasa kuanzia ngazi ya chini kabisa ya familia mpaka ngazi ya juu ili wanafunzi wetu wote wapate elimu bora pamoja na kuwasilisha mipango yenu lakini pia ni vizuri kuwasilisha na changamoto mlizokumbana nazo katika kuandaa mpango huu.
lakini najua kuna uwakilishi wa watu wawili tu ni matumaini yangu kuwa yale mtakayojifunza hapa mtaenda kuwashirikisha jamii yote kwa ujumla ili kuweza kuyatekeleza kwa manufaa ya jamii yetu na kufikia malengo tuliyojipangia.
Hata hivyo mipango inawasilishwa katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru na mipango waliyopanga ni yale mambo watakayofanya kutekeleza mipango yao na baadhi ya mipango yao itajumuishwa kwenye mpango wa serikali ya mwaka wa fedha ujao.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.