Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndugu, Chiza C. Marando amewataka wanufaika wa mikopo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu kuwa waaminifu katika makubaliano waliyoweka wakati wa kuchukua mikopo hiyo.
Marando ameyazungumza hayo katika kikao cha pamoja na wanufaika hao, ambapo walitia saini mikataba ya makubaliano ya kuchukua mikopo hiyo.
Alisisitiza kuwa mikopo hiyo ikafanye kazi kwa ajili ya maendeleo katika Wilaya ya Tunduru na kuwataka wanufaika kuitumia kwa ufanisi na kwa malengo waliyokusudia.
“Kipimo kikubwa cha haya maisha ni uaminifu na uadilifu” Alisema Marando.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Tunduru Bi. Jecelyne Mganga, alisema, vijana saba na vikundi vitatu vimefanikiwa kupata mikopo hiyo kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara zao.
Kwa upande wao, wanufaika wa mikopo wameishukuru serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa uwezeshaji huo na wameahidi kwenda kufanyia kazi kwa bidii ili waweze kulipa mikopo hiyo kwa wakati na kuwanufaisha vijana wengine.
Mikopo hii inatarajiwa kuchangia katika kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na kukuza uchumi wa Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.