Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa kushirikiana na mfuko wa kilimo wa MIVARF( Marketing, Infrastructure ,Value Addition and Rural Financing) wanatekeleza mradi wa ujenzi wa soko na ghala la kuongeza thamani ya zao la mpunga Nakayaya.
Mradi huu wa ujenzi wa ghala na soko mpaka kukamilika utagharimu jumla ya shilingi milioni 904,332,470.00 ambapo mchango wa Halmasahuri ni milioni 41,692,274.00, mchango wa mivarf milioni 844,890,197.00 na mchango wa jamii milioni 17,750,000.00
Mradi wa ujenzi wa ghala na soko la kuongeza thamani zao la mpunga tunduru uliibuliwa na wananchi wenyewe chini ya ushirika wa umwagiliaji wa tunduru kwa kushirikiana na halmashauri na mradi unatarajiwa kukalimika mwezi juni 2017.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.