Kufuatia uchakavu wa miundombinu ya elimu katika shule za Halmashauri ya wilaya Tunduru, serikali iliunda mfuko wa elimu wilaya ili kuweza kukabiliana na changamoto za shule za msingi na sekondari hasa katika vyumba vya madarasa, nyumba za watumishi na matundu ya vyoo.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ilandaa rasimu ya kuanzisha mfuko wa elimu uliopendekezwa katika kukusanya fedha kupitia zao la korosho kwa msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo jumla ya shilingi milioni 608,248,680.00 zimekusanywa kutoka kwa wakulima wa zao hilo waliokatwa jumla ya shiingi 30 kwa kila moja ya korosho katika tan 20,274,956.00 zilizozalishwa.
Kaimu Afisa Mipango Wilaya ya Tunduru Ndg Rudrick Chale akiwasilisha mapendekezo ya matumizi ya shilingi milioni 608 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa klasta ya Mlingoti Mapema leo.
Akiwasilisha matumizi ya fedha hizo katika kikao cha baraza maalum la madiwani la kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 kwa niaba ya Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru Afisa Mipango wilaya Ndg Rudrick Chale alisema fedha hizo zimegawanywa katika matumizi yafuatayo katika kuboresha elimu wilayani Tunduru.
Afisa Mipngo wilaya alisema kuwa kati ya fedha kusanywa elimu msingi wamepata gawio la shilingi milioni 359 na elimu sekondari wametengewa shiingi milioni 240 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu wilayani Tunduru.
Sambamba na hayo alisema kuwa serikali imeona umuhimu wa kitengo cha elimu maalum wilayani Tunduru kimetengewa shilingi milioni 7,248,680 kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali vya wanafunzi hao ikiwemo mafuta ya ngozi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino), kofia na baiskeli za walemavu wa viungo.
Mbunge wa Tunduru Kaskazini Eng Ramo Makani akichangia hoja ya matumizi ya fedha za mfuko wa kuboresha elimu wilayani Tunduru baada ya baadhi ya madiwani kutaka kila kijiji kupata gawio kulingana na uzalishaji.
Akitoa mchango katika kikao hicho mkuu wa wilaya Tunduru Juma Homera aliwataka waheshimiwa madiwani ambao watapata mgawo wa fedha hizi kusimamia miradi kwa karibu na kuacha tabia ya kuwaachia walimu na kamati za shule na tunatoa kipindi cha miezi mitatu hadi kukamilika kama tunavyofanya kwa miradi ya P4R inayotekelezwa na ujenzi wa vituo vya afya inayotekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu na inakamilika.
"nawataka madiwani musimamie miradi iliyopendekezwa na wataalam wetu na tukumbuke hizi fedha ni za wananchi waliokatwa katika mazao yao hivyo tunaomba usimamizi wa pamoja kati ya madiwani na Halmashauri ili kupunguza matatizo ya wanafunzi wanaolundikana kwenye vyumba vya madarasa huko mashuleni"
wahishimiwa Madwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru wakifuatilia sala ya ufunguzi wa baraza inaongwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ambae hayupo katika picha
Juma Homera aliendelea kusema kuwa changamoto ya miundombinu ya Elimu katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ni kubwa sana na kwa awamu ya kwanza mfuko huu utaanza na maeneo ambayo wataalam wamebainisha, lakini ukiangalia katika mgawanyo ulifanywa wataalam umezingatia vigezo vya kitaalam na takribani madarasa sabini yatajengwa hivyo kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera wakiteta na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Mh sikudhani Chikambo katika kikao maalum cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Klasta Tunduru.
Naye mbunge wa Tunduru kaskazini Eng Ramo Makani ni vyema pia kuona pia ni namna gani tunaweza kutumia mazao mengine ambayo yanalimwa wilayani Tunduru katika kuchangia mfuko Elimu na tusiegee tuu kwa zao moja na Korosho ili kuongeza wigo mpana wa kupunguza changamoto za elimu na kukuza Elimu kama mikoa mingine ambayo waliwekeza katika elimu.
Eng Ramo makani aliendelea kutoa hoja upande wa rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 alisema changamoto kubwa ilibainishwa na wataalam ni uosefu wa fedha, hivyo ni vyema madiwani kwa pamoja kuona ni dhairi tunatakiwa kuhamasisha wananchi kuendelea kulima kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji na halmashauri kukusanya zaidi kwani fedha za ndani ndio zinye uhakika wa kuendesha miradi ya maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.